January 17, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais wa Al Hilal avutiwa na shabiki simba, amualika Sudan kutoa Sapoti

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

RAIS wa klabu ya Al Hilal ya Sudan, amevutiwa na mashabiki wa Simba waliowapa sapoti katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika mkondo wa kwanza dhidi ya Yanga SC.

Katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza ambao ulifanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkpa Jijini Dar es Salaam, timu hizo zilitosha nguvu kwa kufungan goli 1-1.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo Rais wa Al Hilal alitangaza ofa ya kuwagharamia mashabiki wa Simba walioishangili timu yao Jumamosi kwa Mkapa kwa kuwalipia nauli na makazi bure ili waende kuishangilia tena Al Hilal nchini Sudan.

Habari hiyo imeenea katika mitandao ya kijamii mbalimbali hapa nchini. Lakini gazeti la majira lilimtafuta mmoja wa mashabiki hao ambaye alionekana katika picha akiishangilia Al Hilal ya Sudan, Iddy Athuman Borry mwenye kauli mbiu isemayo ‘Never give up, Jah Bless’.

Iddy amesema bado hajapata taarifa rasmi kutoka Sudan wala uongozi wa Simba juu ya kupelekwa Sudan lakini ameona taarifa mbalimbali kuhusu suala hilo.

“Nimesikia kwenye mitandao mbalimbali hapa nchini, lakini mpaka sasa napoongea na wewe mwandishi bado sijapata simu kutoka Simba wala nchini Sudani kuwa nahitajika kwenda kuwapa Sapoti,” amesema Iddy.