January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Trump atoa onyo kwa wamiliki wa TikTok na WeChat

Mitandao ya kijamii ya TikTok na WeChat inayomilikiwa na Wachina utazuiwa ndani ya siku 45 zijazo kama isipouzwa kwa Wamarekani ndani ya siku hizo.

Hayo yamebainishwa na Rais wa Marekani Donald Trump ambapo amepanga kuzuia mitandao hiyo Septemba 15, ikiwa haitauzwa.

Aidha, Wahusika wa mitandao hiyo wapo katika maongezi na kampuni ya kimarekani ya Microsoft.

Sababu za Rais Trump kuifunga mitandao hiyo imetokana na tuhuma za kuiba taarifa za watumiaji wake na kupeleka kwa Serikali za China ambapo hadi sasa TikTok ina watumiaji zaidi ya milioni 100 nchini Marekani