Na David John, Timesmajira Online, Mbeya
RAIS Samia Hassan Suluhu amesema Chuo cha VETA Mbarali kitafungua fursa kwa wanambarali kupata mafunzo ya ufundi Stadi na kwenda kutoa huduma kwa wananchi.
Hayo ameyasema wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika Chuo cha VETA cha Wilaya ya Mbarali kilichojengwa katika Kijiji cha Mwaganga wilayani humo mkoani Mbeya.
Rais Samia Hassan Suluhu amesema mafundi umeme watapatikana hapo washonaji , mafundi uchomeleaji , watu wa urembo nao watapatikana ni fursa kwa vijana kwenda kusoma chuo hicho.
Amesema Rais Samia Kozi fupi zitaanza septemba na kozi ndefu mwakani ambapo baada ya kukamilika atazindus mwenyewe na kupata muda wa kuongea na wanambarali.
Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema Wilaya ya Mbarali ni miongoni mwa Wilaya 25 wanufaika wa mradi wa ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vya Wilaya ulioanza kutekelezwa mwaka wa fedha 2019/2020. Ujenzi wa vyuo hivi ulianza kupitia mradi wa ambapo Serikali ilitenga Shilingi za Kitanzania Bilioni 40, sawa na Shilingi Bilioni 1.6 kwa kila Chuo kwa ajili ya kuanza kazi za ujenzi.
Profesa Mkenda amesema kupitia Mpango wa maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 Serikali ilitenga tena jumla ya Shilingi bilioni 28.76 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyuo hivyo pamoja na gharama za kutengeneza samani.
Amesema vyuo vya vinajengwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ambapo ujenzi wa chuo cha Mbarali unatekelezwa na kusimaiwa kupitia Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Mbeya (VETA Mbeya).
Aidha, Chuo cha VETA Mbeya pia kinatengeneza samani kwa ajili ya chuo hiki na Chuo cha Ufundi Stadi cha wilaya ya Chunya huku
Amesema chuo hicho kinatarajiwa kuhudumia wakazi wote wa Wilaya hii na maeneo ya jirani na mradi ujenzi wa chuo hicho una jumla ya majengo kumi na saba (17) ambayo ni Jengo la utawala, Karakana 4, Jengo la madarasa, Mabweni mawili Bwalo la chakula, Majengo tatu ya Maliwato, Nyumba ya Mkuu wa Chuo, Nyumba ya familia mbili za watumishi, Jengo la mitambo ya umeme, Jengo la stoo na Jengo la ofisi ya walinzi.
Profesa Mkenda amesema chuo cha mbarali kikikamilika kinatarajiwa kuanza na fani tisa za muda mrefu na mfupi ambapo jumla ya wanafunzi 240 wanatarajiwa kudahiliwa kwa mwaka kati yao wanafunzi 144 watakuwa wa bweni na 96 watakuwa wa kutwa pia Chuo kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi wapatao 500 wa kozi za muda mfupi kwa mwaka, hivyo kufanya idadi ya jumla ya wanafunzi wanaodahiliwa kuwa 740 kwa mwaka.
Amesema Fani za muda mrefu na mfupi zitakazotolewa kwa awamu ya kwanza ni Uhazili na Kompyuta,
Ubunifu wa Mitindo,Ushonaji na teknolojia na nguo,
Uashi Umeme wa Majumbani na viwandani, Ufundi wa Magari,Ufundi wa zana za Kilimo, Uchomeleaji na Uungaji Vyuma,
Mafunzo ya Udereva,
Ufundi wa kutengeneza pikipiki na pawatila.
Profesa Mkenda amesema mradi ulianza kutekelezwa tarehe 8 Machi, 2020 hadi sasa utekelezaji wa mradi huu umefikia asilimia 95 ambapo majengo yote 17 yamekamilika na kubakiwa na kazi za usambazaji wa umeme, maji, barabara na ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua.
” Ni matarajio ya Mamlaka kuanza kufanya taratibu za usajili wa wanafunzi ifikapo mwezi Septemba, 2022 kwa lengo la kuanza kutoa mafunzo ifikapo Januari, 2023. Aidha, utoaji wa mafunzo ya kozi za muda mfupi zisizohitaji mitambo mikubwa na vifaa yataanza kutolewa mwezi Septemba 2022 kulingana na mahitaji ya Wilaya hii pamoja na shughuli za kiuchumi zinazofanyika katika eneo hilo.
Amesema gharama za ujenzi wa mradi huo awamu ya kwanza Kiasi cha Shilingi 1,600,000,000 (Bilioni moja na milioni mia sita) kilitolewa na Serikali kupitia mradi wa kwa ajili ya kuanza ujenzi na awamu ya pili Serikali ilitoa kiasi cha Shilingi 631,527,204 kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 kwa ajili ya kumalizia ujenzi, na hivyo kufanya Kiasi cha Shilingi 2,231,527,204.00 kuwa kimetolowa na kutumika katika mradi huu.
Utengenezaji wa Samani
Samani kwa vyuo vyote 25 zinatengenezwa kwa jumla ya Shilingi Bilioni 8.76 ikiwa ni sehemu ya Shilingi Bilioni 28.76 za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19. Jumla ya samani mbalimbali 39,750 zinatengenezwa kwa ajili ya vyuo 25 vya Wilaya zikihusisha za maofisini, madarasani, karakana, mabweni ya wanafunzi na bwalo la chakula. Utengenezaji umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Agosti 2022.
Hata hivyo amesema utengenezaji wa samani hizo unafanyika katika Kiwanda cha Samani cha VETA kilichopo Mkoani Dodoma na katika Karakana za Vyuo vya VETA vilivyopo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Mbeya, Lindi, Mwanza, Shinyanga, Tabora na Kigoma.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini