Na Zena Mohamed,TimesMajiraOnline,Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka bodaboda na bajiji nchini kutokukubali kutumika katika vitendo vya wizi na uporaji wanapofanya shughuli za usafirishaji.
Rais Samia amesema hayo leo kwa njia ya simu wakati wa kongamano la kuimarisha ushiriki wa waendesha Bodaboda na Bajaji katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu liliandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Ambapo amewataka waendesha bodaboda na bajaji nchini kutambua kuwa wao ni wasafirishaji wa kitaifa hivyo watumie nafasi hiyo kufanya mambo mema kwa jamii ikiwemo kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makazi na kuacha ukwapuaji wa mizigo ya watu.
“Nawaomba muache tabia ya wizi na kukwapua mizigo ya watu hasa wadada baadhi yenu wamekuwa wakikwapua mikoba ya kina dada hivyo nawasihi viongozi wenu wakasimamie hilo msitumie bodaboda vibaya ninyi ni watu muhimu sana katika usafirishaji,
“Nyinyi ni maafisa usafirishaji wa Taifa wa kusafirisha mizigo ya watu na watu nawaomba msifanye ujambazi huo ndio usafiri wetu wanyoge niwaombe sana najua kazi yenu kuna waosomi ndani yake niwambie tu mama yenu nipo na nyinyi mkayafanie kazi mnayoyapata hapo,nendeni mkahamasishe zoezi la sensa ya watu na makazi kwa sababu tukijua idadi ya watu tutaweza kuwasaidia kwa pamoja na maendeleo ya taifa yataonekana kwa ujumla nendeni mkahamasishe watu kushiriki zoezi hilo”amesema.
More Stories
Madiwani Ilala watoa chakula kwa watoto yatima
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano