Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dar
RAIS Samia Suluhu Hassan ameanza ziara ziara ya kikazi nchini Kenya kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais wa Kenya, William Samoei Ruto.
Rais Samia ameanza ziara hiyo leo ambapo ameshiriki hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya Raila Odinga, anayewania nafasi ya
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU).
Kwa mujibu wa taarifa iliyoyotolewa jana Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo itafanyika Ikulu ya Nairobi na kuhudhuriwa na Wakuu wa Nchi mbalimbali.
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya