December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia: Tutaongeza mishahara mwakani

Na Penina Malundo,timesmajira,Online

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kwa mwaka huu serikali haitaweza kuongeza mishahara kwa wafanyakazi kutokana na athari za ugonjwa wa Corona kuathiri nchi nyingi kiuchumi.

Akizungumza hayo leo jijini mwanza katika Sherehe za maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani Mei Mosi,amesema miongoni mwa nchi  zilizoathiriwa ni pamoja na Tanzania ambapo imeathiri uchumi wake kwa kushuka asilimia 6.9 hadi 4.7 hivyo kushindwa kuongeza mishahara hiyo.

“Mwakani siku kama ya leo nitakuja na package nzuri ya nyongeza za mishahara kwa watumishi,hivyo naagiza haraka kwa kuundwa kwa Bodi za Mishahara ili nifahamu kabisa tena mapema kuwa mwakani napandisha mishahara kwa kiwango gani,”amesema