December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia: tumesaini mikataba ya Trilioni 1.9

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9. Hafla ya utiaji saini Mikataba ya kuimarisha Gridi ya Taifa na usambazaji wa umeme Vijijini imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.
Wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9 Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia Utiaji Saini wa Mikataba ya Utekelezaji wa Miradi Mahsusi ya Umeme yenye thamani ya Shillingi trilioni 1.9 ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha Serikali inadhamiria kusambaza umeme Nchi nzima.

Ameyasema hayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kushuhudia utiaji saini mikataba ya Gridi Imara yenye thamani ya shillingi Trillioni 1.9, Leo Februari 14, 2023 Ikulu jijini Dar es salaam

“Kawaida ya maendeleo ni wivu, miaka 10, miaka 15 nyuma Bungeni hakukuwa na kilio sana cha umeme, kilio kilikuwa maji, maji mpaka tumefanyia kazi maji tumefikia pazuri tumefikia 80% si haba lakini kilio sasa kikubwa ni umeme”

“Kwa kawaida ya Binadamu ukiona Kijiji cha Jirani kuna umeme umapata wivu, maendeleo haya ukimuonjesha mmoja na wengine nao wanakuja juu kwahiyo kilio hicho tumekipokea nasi tumejipanga kulifanyia kazi suala la kusambaza umeme Tanzania nzima”

“Miradi ikikamilika hasa huu wa gridi utaongeza hata usalama Vijijini, wale chinjachinjw wanaokata mapanga Watu ni kwasababu ya giza tukipeleka umeme hakuna wa kupenya na kufanya vurugu nchi itaimarika pia kiusalama”

“Huudma ya Tehama itawafikia Vijiji, tukipeleka umeme Vijijini, Tehama ikiingia Vijini tutahamaisha maendeleo Vijijini”

“Upande wa REA pamoja na kazi kubwa tuliyofanya bado tuna kazi kubwa ya kupelekea umeme vitongojini, wakati tunajisifia kwamba December mwaka huu Vijiji vyote vitakuwa na umeme kule kwenye vitongoji tuna kazi kubwa, tunakwenda kufanya kazi hii ya kupeleka umeme hadi kwenye vitongoji”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9, Ikulu Jijini Dar es Salaam.