December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia, Nyusi watembelea Banda jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama wakati akitoa maelezo kuhusu Mfumo wa Ufuatiliaji wa mwenendo wa majanga na tahadhari ya mapema (MYDEWETRA) wakatiwalipotembelea katika Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizochini yake katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) tarehe 03 Julai, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Maonesho hayo ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam (Sabasaba) yamefunguliwa rasmi leo (Julai 3, 2024) na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi pamoja na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.