Na Daud Magesa, Timesmajira Online, Mwanza
RAIS Samia Suluhu Hassan,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi,mashindano ya kimataifa ya kusoma na kuhifadhi Kuran(Quran),yaliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).
Mashindano hayo yatakayofanyika Agosti 31, mwaka huu,uwanja wa Benjamin Mkapa,ambayo yatashirikisha wasichana wa dini ya kiislamu yakiwa na malengo matatu.
Sheikh wa Mkoa wa Mwanza,Alhaji Hassan Kabeke,akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza,Agosti 16,2024,amewataka wazazi kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika mashindano hayo ya kuhifadhi Kuran.
Katibu wa taasisi ya Muslim World League ya nchini Saudi Arabia,Mohamed
Bdulkarim Al-ssa,ni miongoni mwa watakaohudhuria mashindano hayo,ambayo yanahamasisha usomaji wa Kuran na kuingiza upendo wa Kuran hiyo tukufu katika nyoyo ikiwa ni pamoja na kuihifadhi.
Kupitia mashindano hayo wataenzi mchango wa watu waliotangulia mbele za haki,walioutoa katika kuisoma na kuhifadhi Kuran.
Kwa mujibu wa Sheikh Kabeke,mradi wa kurekodi Msahafu kwa Qira’at zote kumi utazinduliwa,ikiwa ni hatua ya kuongeza ufahamu,usomaji sahihi wa Kuran tukufu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA) Mkoa wa Mwanza,Amina Masenza,amesema mashindano hayo ya kusoma na kuhifadhi Kuran ni fursa,inarithisha kizazi hadi kingine,wasichana wenye uwezo wakashiriki kwa sababu yanatia hamasa kwa wasikilizaji.
“Ni jambo la kufurahisha sisi wasikilizaji,washiriki watajifunza na kuja kufundisha namna bora ya kughani Kuran na taratibu zake,rai yangu kwa wazazi wenye watoto wa kike wawape fursa wakashiriki mashindano
hayo,”amehimiza.
More Stories
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu