December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia Mgeni Rasmi sherehe za Mei Mosi, Mwanza

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mwaka huu ambapo kitaifa yatafanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema leo Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU, Gerson Msigwa, Maadhimisho hayo yatafanyika leo(01/05/2021) kuanzia saa 3:00 asubuhi ambapo atalihutubia taifa, atapokea maandamano, risala ya wafanyakazi, atatoa zawadi kwa wafanyakazi bora na atatoa zawadi kwa washindi wa mashindano ya Mei Mosi.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Samia kuhudhuria kama mgeni rasmi katika sherehe hizi toka aape kuwa  Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ambapo ni jana tu amepitishwa kwa kishindo kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.