Na Penina Malundo
RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 36 ya Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA) yanayotarajiwa kufanyika Novemba 28 na 29 Mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere.
Akizungumza na waandishi wa habari Jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dkt. Rose Reuben alisema licha ya kuanzishwa miaka 36 iliyopita ,Chama hicho Kiko Imara hadi sasa na kina jumla ya wanachama 255 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Amesema katika maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine wanatarajia kuzindua Jarida la Sauti ya Siti ambalo lilisimama uchapishwaji wake tangu Mwaka 2017 ,pamoja na kuzindua ripoti ya rushwa ya ngono na Ukatili wa Kijinsia ndani ya vyombo vya habari.
“Kwa siku mbili hizi za maadhimisho tunatarajia kuwa na wageni mbalimbali wakiwemo kutoka katika sekta ya Habari na Jinsia, msemaji wa Serikali, viongozi wa dini, viongozi wa mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali,wamiliki wa vyombo vya habari, Wahariri pamoja na waandishi wa habari,”amesema na kuongeza
“Pia katika maadhimisho hayo tunatarajia kutoa tuzo kwa mwanahabari aliyefanya vizuri katika masuala ya afya ya Uzazi na kutoa zawadi Maalum ya kutambua na kuthamini Mchango wa waasisi wa TAMWA 13,”amesisitiza.
Aidha amesema maadhimisho ya Mwaka huu yanaakisi safari ya miaka 36 ya TAMWA ambayo yameendelea kujikita katika kuhamasisha upatikanaji wa haki za wanawake na watoto wa kike nchini.
“Maono yetu ni kuwa jamii ya kitanzania iliyo na amani na inayoheshimu haki za binadamu kwa mtazamo wa Kijinsia,”amesema.
Akizungumza miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana na TAMWA ni pamoja na bunge mwakan1988 kutunga sheria ya masuala ya kujamiiana lengo ikiwa ni kuzuia Ukatili na kulinda heshima,hadhi,utu na haki za wanawake na watoto.
Amesema nyingine ni kuondolewa kwa sheria ya wanawali ya Mwaka 1985 ambapo Msichana alipata mimba alifungwa jela na kama mwanafunzi hakuruhusiwa kurudi shule tena kusoma.
“Sheria hii iliondolewa Jana jitihada na ushawishi qa Rais Samia ambaye kwa wakati ule alikuwa Waziri Zanzibar aliyekuwa na dhamana ya masuala ya Kijinsia,”amesema
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua