Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa upanuzi wa kiwanda cha sukari cha K4.
Hii ni Katika mkakati wa kuunga mkono juhudi za Serikali kuhakikisha nchi inakua na utoshelevu wa bidhaa ya Sukari.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Sukari Kilombero, Derick Stanley alisema tukio hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 4 Agosti Mwaka huu.
Stanley amesema gharama ya upanuzi wa mradi huo itakuwa ni Sh 744 bilionipunde mradi utakapokamilika mwezi Juni 2025.
Amesema kukamilika kwa mradi huo kutaongeza uwezo wa kampuni hiyo katikakuzalisha sukari kutoka tani 126,000 kwa mwaka hadi kufikiatani 271,000 kwa mwaka ifikapo mwaka 2025.
“Kiwanda hiki cha K4 kilianza kujengwa miaka miwili iliyopita, ambapo ni kiwanda cha kisasapia ni kiwanda kinachoongoza kwa ukubwa, Afrika Mashariki. Kukamilika kwa kiwanda hiki kutapunguza changamoto za uhaba wa Sukari hapa nchini, hivyo kuisaidia Serikali yetukutoagiza Sukari nje ya nchi”.
Ndugu Derick Stanley ameongeza kuwa “Mradi unaenda kuletamapinduzi makubwa katika sekta ya Uchumi hapa nchini, hiiina ambatana na dira ya Serikali kwamba ifikapo mwaka 2025 nchi ya Tanzania iwe na utoshelevu wa Sukari ya matumizi yamajumbani”.
Amesema kupitia kiwanda hiko cha K4 kutakuwa na ongezeko la mapato kwa wakulima wa bonde la Kilombero kutoka shilingi za kitanzania bilioni 75 hadi kufikia takribani shilingi bilioni 165 kwa mwaka, Sambamba na ongezeko la idadi ya wakulimakutoka 8,000 hadi kufikia takribani 16,000.
Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano na Mahusiano kwawadau, Victor Byemelwa amewahimiza wananchi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi siku hiyo ili kushuhudiatukio hilo la kihistoria ambalo linaenda kuinua maisha yawakulima kupitia uzalishaji wa miwa.
Naye Meneja wa Masuala ya Biashara wa Kampuni ya Sukari Kilombero Willa Haonga amewataka akina mama kuchangamkia fursa ya mradi huu kwani tafiti zinaonesha kuwawanaume ndio wanaongoza kwa biashara ya kilimo cha mua.
Amewataka akina mama kuchangamkia fursa hii ili kujiinuakiuchumu na kuunga juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia SuluhuHassan, ambaye amekua mstari wa mbele katika kuwainuawanawake.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato