January 30, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia kuzindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2024 Toleo la 2023

Na Zena Mohamed, Timesmajiraonline, Dodoma

RAIS Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 Toleo la 2023 Mitaala iliyoboreshwa, Februari Mosi mwaka huu baada ya kukamilika kwake na kuidhinishwa kwa ajili ya kuanza kutumika rasmi.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda aliwaambia waandishi wa habari jijini hapa leo katika mkutano wake kuhusu kubadilishwa kwa tarehe ya uzinduzi huo ambao ulikuwa ufanyike Januari 31 mwaka huu na badala yake utafanyika Februari Mosi mwaka huu.

Maboresho ya Sera ya hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia aliyoyatoa kwa nyakati tofauti juu ya kufanya mapitio ya Sera ya elimu na Mafunzo ya 2014 pamoja na kufanya maboresho ya mitaala ya elimu katika ngazi mbalimbali ili ijikite katika kutoka elimu ujuzi badala ya elimu ya taaluma pekee.

Mkutano huo unaotarajiwa kuhudhuriwa na watu 3000 ambao ni wadau mbalimbali wa elimu kutoka na nje ya nchi, utakaofanywa na Rais, Samia Februaro Mosi mwaka huu jijini Dodoma.

Prof.Mkenda alisema tayari wageni mbalimbali wameshaanza kuwasili jijini Dodoma kwa ajili ya shughuli hiyo kutoka Tanzania Bara na Visiwani.

Alisema kukamilika kwa sera hiyo na mitaala yake iliyochukua muda wa miaka mitatu kufanyiwa mapitio na marekebisho kunakwenda kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini na utekelezaji wake utakwenda kwa awamu.

“Baada ya maelekezo ya Rais wetu, kazi ilianza, ya kufanya mageuzi na mapitio ya sera na vilevile mapitio ya mitaala, kazi iliyochuyokua takribani miaka mitatu, kazi hii ilifanywa kwa namna shirikishi, kwa kushirikisha wadau mbalimbali, watalam wa elimu, walimu, wanafunzi, wananchi na maoni yalikuwa yakikaribishwa nyakati zote kwa ajili ya kupata namna ya kusonga mbele,”alisema Profesa Mkenda.

Waziri huyo alifafanua kuwa mchakato huo pia ulihusisha kujifunza kwa wenzao kutoka nchi mbalimbali na timu ambazo zimefanya kazi hiyo zilitembelea baadhi ya nchi kwenda kuangalia wanachokifanya ili na Tanzania ili iuweze kuona namna ya kuboresha elimu hiyo.

“Napenda kuwaarifu kuwa kazi ya kupitia sera ilikamilika, sasa tunayo sera ya elimu haoa nchini ambayo inaitwa kwa kirefu Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 Toleo la 2023, na sera hiyo imesha idhinishwa na Rais Samia, kupitia kikao cha baraza la mawaziri.

Alisema sambamba na Sera, mitaala nayo imefanyiwa mapitio ili kuendana na sera ambayo wanayo hivi sasa.

“Tuna mitaala mipya ambayo tunaitekeleza kwa awamu, suala hili ni kubwa, mageuzi yaliyoko kwenye sera ni makubwa sana yanatekelezwa kwa awamu na tutakuwa tunaona kila mwaka hatua ambazo zinachukuliwa,”alisisitiza waziri.

Waziri huyo alieleza kuwa ni mabadiliko ambayo yatagusa vizazi na vizazi, ukamilifu wa utekelezaji wake kuanzia elimu ya awali mpaka kidato cha sita utachukua muda, kwasababu tulianza hatua kwa hatua elimu ya awali, darasa la kwanza, darasa la Tatu, kidato cha kwanza na mengineyo.

Profesa. Mkenda ni hatua kubwa ambayoi itabadilisha muelekeo wa nchi katika sula la elimu.

“ Tunasikia watu bado wanatoa michango kuhusu mabadiliko ya elimu kuna hoja mbalimbali ambazo zinazungumzwa na sisi tunazifuatilia, majibu karibia ya hoja zote zimejibiwa katika sera na mitaala mipya, kwa mfano mjadala mkubwa unaoendelea sasa hivi hapa nchini ni kuhusu somo loa kiingereza.

Ukienda kwenye sera utaona suala la lugha, ukienda kwenye mitaala ufundishaji wa lugha, tunasikia watu wanazungumza suala la ‘artificial intergence’ ni suala kubwa sana,”alisema.

Alisema ukienda kwenye sera utaona masuala ya Tehama na mambo yote yanayohusiana na Tehama yalivyozungumzwa, na ukija kwenye mitaala utaona utekelezaji wake unavyofanyika na kuna suala kubwa sana la sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati ambavyo vinazungumzwa sana kwa haki na kuelekeza kwamba wanatakiwa wafanye nini.

“Ukienda kwenye sera utaona masuala hayo yanavyoshughulikiwa, ukienda kwenye mitaala utaona jinsi ambavyo yanatekelezwa, kuna masuala ya kumuandaa mwanafunzi, sio tu kwenye ubora wa elimu lakini kuna ujuzi wa kumuandaa kwenye dunia ya sasa na mabadiliko makubwa yanayotokea duniani kwenda mbele, ukienda kwenye sera utakuta masuala hayo yanavyoshughulikiwa, ukienda kwenye mitaala utaona jinsi yanavyotekelezwa,”alisisitiza.

Alisema viongozi wakuu na wandamizi wa nchi wamealikwa na watashiriki katika tukio hilo na wadau mbalimbali wakiwemo sekta ya elimu pia kutakuwa na maonesho mbalimbali ya elimu.

“Tunawalika Watanzania wote wale watakaokuja wajiandikishe kwa sababu tumetoa furlsa, ya kujisajili kushiriki hivyo tunatarajia watafanya hivyo mapema,pia tunawaalika watanzania wote kufuatilia kwenye vyombo vya habari shughuli ya uzinduzi huo ambapo taarifa itatolewa,”alisisitiza Profesa. Mkenda.