January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia kuongoza Mkutano wa FOCAC China

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline, China

RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika na China (FOCAC) katika mkutano unaotarajiwa kuaanza kuanza leo Septemba 4 hadi 6, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa jana ilieleza kuwa Rais Samia atahutubia ufunguzi wa mkutano wa FOCAC na pia atafanya mazungumzo na Rais China, Mhe. Xi Jinping na kushuhudia uwekaji saini wa Hati za Makubaliano ya Uboreshaji wa Reli ya TAZARA.

Aidha, atakutana na makampuni na wawekezaji kutoka China ili kuhamasisha uwekezaji zaidinchini Tanzania.