January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia kuhudhuria,Mkutano wa SADC

Na Mwandishi Wetu,Timesmajira

RAIS Samia Suluhu Hasan, anatarajia kuhudhuria Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika  Agosti 17, 2024 mjini Harare, Zimbabwe.

Rais Dkt. Samia anaondoka nchini leo Agosti 15, 2024
kuhudhuria Mkutano huo wenye kauli mbinu:  “Kukuza ubunifu ili kufungua
fursa za ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu kuelekea SADC yenye
viwanda.”

Katika Mkutano huo, Rais Dkt. Samia anatarajia kuchaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC akipokea kutoka
kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Hakainde Hichilema anayemaliza muda
wake.