*Kuanzia ziara kwa mwaliko maalum wa Rais wa nchi hiyo leo,
ni baada ya miaka 14 kupita, makubwa yatarajiwa sekta tofauti
Na Penina Malundo,Timesmajiraonline,Dar
RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajia kuanza ziara yake ya kitaifa leo nchini Uturuki hadi Aprili 21, 2024 kwa mwaliko maalum wa Rais wa Nchi hiyo, Recep Tayying Erdogan.
Rais Samia anakwenda ziara hiyo itakayochukua siku tano, ikiwa ni miaka 14 imepita tangu Rais wa Tanzania alipotembelea nchi hiyo, huku miaka saba tangu Rais wa nchi hiyo, Erdogan alipotembelea Tanzania Januari 2017.
Uturuki ni kati ya nchi zilizoweka msisitizo katika mahusiano yake na nchi za Afrika, jambo lililojenga muingiliano wa watu kati ya nchi hizi mbili.
Wafanyabiashara wengi wa Tanzania wamekuwa wakienda kukununua bidhaa Uturuki na Tanzania imekuwa ikiuza bidhaa nyingi huko.
Ziara hii ina lengo la kuimarisha mahusiano ya kidplomasia, kibiashara na kisiasa kati ya nchi hizo mbili pamoja na kuimarisha mahusiano ya kibiashara na kiuchumi, kwani Tanzania inahitaji mitaji,teknolojia na wawekezaji.
*** Katika Sekta ya Uwekezaji
Uwekezaji wa kampuni za Uturuki Tanzania bara una thamani ya takribani dola milioni 414,23 za Kimarekani kwenye sekta za usafirishaji, uzalishaji na utalii ambao umetoa ajira 6,062.
Kwa Upande wa Zanzibar ,Uturuki imefanya uwekezaji wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 96.4 kwenye sekta ya utalii na kutoa fursa za ajira 719.
*** Biashara na utalii
Katika upande wa Biashara na Utalii, Biashara kubwa Tanzania inayouza Uturuki ni kahawa, nazi, tumbaku ghafi, minogu ya samaki ,dhahabu,mchele na maharage ya soya ambapo huuza bidhaa zenye thamani ya wastani wa Dla za Marekani milioni 15.99 kwa mwaka.
***Sekta ya Elimu
Kila mwaka Serikali ya Uturuki hutoa udhamini kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka Tanzania kusoma Uturuki kuanzisha shahada ya kwanza hadi shahada ya uzamivu,Udhamini wa vyuo vikuu vya Uturuki ni katika masomo ya Afya,Uhandisi ,Uchumi ,Biokemia,Famasia ,Kilimo na Sayansi ya Jamii.
***Sekta ya afya
Tanzania na Uturuki zina ushirikiano mkubwa kwenye sekta ya afya, ambapo Uturuki imekuwa ikitoa misaada ya vifaa vya kitabibu na idadi kubwa ya Watanzania hupata matibabu katika hospitali za Uturuki.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa