January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia kuelekea nchini Brazil kushiriki mkutano wa G20

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) tarehe 16 Novemba, 2024 kabla ya kuelekea Rio de Janeiro nchini Brazil kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa kundi la G20.

Rais Dkt. Samia amealikwa na Rais wa Brazil  Luiz Ińacio Lula da Silva ambapo pamoja na mambo mengine, atashiriki mijadala inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya njaa na umasikini, kuchochea maendeleo endekevu na matumizi ya nishati mbadala.