Na WAMJW-MWANZA
RAIS wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameiagiza wizara ya Afya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuendelea kufanya utafiti wa chanzo cha ugonjwa wa Saratani ambao unaendelea kuathiri watu wengi katika Mikoa ya kanda ya ziwa hasa wanawake.
Agizo hilo amelitoa leo Jijini Mwanza katika maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda – Bugando.
Mhe.Samia amesema kuwa inasikitisha kuona idadi ya wagonjwa wa saratani inaongezeka kwa kasi kubwa kutoka wagonjwa 1200 mwaka 2019 hadi kufikia wagonjwa, hali inayokwamisha uzalishaji mali na kufifisha jitihada za Serikali katika kuleta maendeleo.
Amesema kuwa, licha ya Watafiti kubaini kuwa baadhi ya viashiria kama Uchafuzi wa mazingira katika vyanzo vya maji ya kemikali yanayotoka kwenye migodi ya madini hupelekea ugonjwa huo, lakini ipo sababu ya kuchunguza zaidi kwani tatizo hilo huwakumba wanawake zaidi. Alisisitiza.
Mbali na hayo Mhe Samia amesema, Serikali kwa kushirikiana na kanisa katoliki imeboresha huduma za afya katika hospitari ya Rufaa Kanda ya Bugando kwa kuongeza vitanda kutoka 550 hadi 950.
Aliendelea kusema kuwa, kila mwaka Serikali hutoa kiasi cha shilingi Bilioni 20 kwaajili ya kulipa mishahara kwa Watumishi 1200 wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, ikiwa ni sehemu ya mashirikiano katika utoaji huduma za afya kwa wananchi.
Aidha, Serikali hutoa ruzuku ya dawa kwa wastani wa shilingi Bilioni 1 kila mwaka na zaidi ya shilingi Milioni 200 kila mwaka kwaajili ya uendeshaji wa hospitali, huku akisisitiza hivi karibuni Serikali imetoa shilingi Bilioni 4.2 kwa ajili ya kuboresha huduma za kibingwa.
Hata hivyo Mhe. Samia amesema, Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 4.2 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba huduma za Dharula na wagonjwa mahututi, ikiwa ni moja ya Mkakati wa Serikali katika kuboresha Sekta ya Afya nchini.
Pia, Mhe. Samia amewataka Wataalamu kujenga tabia ya kutunza vifaa na mashine zinazonunuliwa kwaajili ya kutoa huduma za afya, ikiwemo mashine hii ya MRI, hali itayosaidia kupunguza gharama ya kisafirisha wagonjwa kwenda nje ya nchi kwaajili ya matibabu.
Mbali na hayo, ameagiza Wizara kusimamia fedha zilizotolewa kuboresha miradi ya ujenzi huku akiahidi kuendelea kutoa ajira za Watumishi kadiri inavyowezekana.
Nae, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dkt. Dorothy Gwajima amemshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuikuza Sekta ya Afya nchini ikiwemo maboresho ya miundombinu, dawa vifaa pamoja na vifaa tiba.
Dkt. Gwajima amewataka wananchi wa mikoa ya kanda ya Ziwa kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya UVIKO-19 kwa ili kuimarisha kinga ya mwili na kuweza kupambana dhidi ya ugonjwa huo.
Aliendelea kusisitiza kuwa, Serikali ipo mbioni kupitisha Sheria ya Bima ya Afya kwa wote itakayo toa fursa kwa kila mwananchi kupata huduma katika kituo chochote kutolea huduma ya afya na kupunguza gharama za matibabu nchini.
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili