Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa nchi za afrika kuendeleza vijana kufikia ndoto zao ili kukuza rasilimali watu kwa maendeleo ya uchumi Kwa nchi za Afrika
Suala la maendeleo ya rasilimali watu Afrika haliwezi kuja kwa kubahatisha na haina mbadala, lazima kuwe na mipango madhubuti ya kuhakikisha rasilimali watu Afrika inaendelezwa kwa manufaa ya bara hili na kwa maendeleo yetu
Hayo yamesemwa leo Julai 26, 2023 kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika wenye lengo la kujadili kuhusu mtaji wa rasilimali watu amesema Afrika Ina idadi kubwa ya vijana hivyo hiyo ni fursa ya pekee katika mageuzi ya uchumi.
“Idadi kubwa ya vijana tuliyonayo ni fursa ya kipekee katika ukuaji wa uchumi katika bara letu kuliko kuwaacha vijana hawa kwenda kutafuta fursa ulaya na kupata tabu njiani tuwawezeshe kwani maisha Bora yapo Afrika”amesema Dkt Samia
“Kwetu sisi tujiulize kuwa bara letu la Afrika tulilolirithi kutoka kwa waasisi wetu waliotafuta uhuru ndilo bara tunalotaka kuwarithisha vizazi vijavyo au wajukuu wetu, Je Afrika tunayoijenga leo ni yenye uchumi endelevu au uchumi unaodumaa” – amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
“Lazima tuwafundishe watoto wetu kuhusu uzazi wa mpangilio, Afrika population yetu ni kubwa sana na inaweza ikatuletea tija au ikaleta mambo yasiyofaa kama hatukuitumia vizuri”
Amesema katika kuhakikisha Taifa la Tanzania linalinda na Kutunza rasilimali watu nchi imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kutenga Fedha kwenye Afua za lishe na kulinda Afya ya mama na mtoto lakini pia kuanzisha vituo vya watoto.
Ameongeza kuwa uanzishwaji wa mfuko wa kupunguza umaskini TASAF lakini pia mfuko wa kusaidia vijana kiuchumi pamoja na kuwarudisha wanafunzi waliopata mimba shuleni baada ya kujifungua.
Aidha Rais Samia amesema uwekezaji wa rasilimali watu ni wajibu wa kimaadili ili kujenga Afrika yenye uchumi wezeshi Kwa kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao.
Kwa upande wake Makamu wa rais wa Benki ya Dunia Dkt. Victoria Kwakwa amesema nchi za Afrika zinachangamoto kubwa ya elimu Kwani watoto wa Afrika kusini mwa jangwa la sahara asilimia 80 hawajui kusoma Wala kuandika.
Amesema maboresho katika sekta ya elimu yatasaidia kukuza mtaji wa rasilimali watu katika nchi za Afrika.
“Uganda imekua ya kwanza Kwa kuondoa udumavu kwenye maendeleo endelevu na Kenya imeboresha kwa asilimia 50 katika sekta ya elimu”amesema Kwakwa
Aidha Dr. Kwakwa ameipongeza Tanzania Kwa kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu Kwa kuwarudisha shuleni wanafunzi waliopata mimba shuleni baada ya kujifungua.
Sambamba na hayo amesema zàidi ya asilimia 50 ya walimu hawafundishi vizuri hivyo Kuna haja ya kutenga Fedha Kwa ajili ajili ya kuboresha miundombinu ya walimu ili kufikia maendeleo na kuboresha sekta ya rasilimali watu.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi