January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia azindua ofisi ya CCM tawi la Chaani

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan leo Januari 17,2024 amezindua ofisi ya Chama hicho Tawi la Chaani Masingini iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa Ziara ya Kikazi Visiwani Zanzibar.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi huo, Rais Dkt, Samia ametoa wito kwa Wanachama kujiandaa na chaguzi lakini pia kudumisha Umoja na Mshikamano.

Ujenzi Wa ofisi hiyo umegharimu Shilingi Milioni 248 ambapo ndani yake Kuna ofisi za Jumuiya zote za Chama.