January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia azindua Daraja la Ruaha Mkuu

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo amezindua Daraja la Ruaha Mkuu lenye urefu wa mita 133 katika barabara ya Mikumi- Kidatu – Ifakara sehemu ya Kidatu – Ifakara kilometa 66.9 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Morogoro.

Ujenzi wa Daraja la Ruaha Mkuu limejengwa sambamba na barabara ya Kidatu – Ifakara kwa kiwango cha lami.

Ujenzi ulianza 02 Oktoba 2017 na kukamilika 30 Juni, 2024 kwa gharama ya Shilingi Billion 157.15, ikihusisha ujenzi wa barabara, daraja, usimamizi na fidia ya mali zilizoathiriwa na mradi.

Daraja hilo limejengwa na Mkandarasi Reynolds Construction Company – RCC ya Nigeria na Mhandisi Mshauri kutoka Kitengo cha Uhandisi (TANROADS Engineering Consulting Unit – TECU).

Usanifu na maandalizi ya nyaraka za zabuni ulifanywa na Kampuni ya kihandisi ya Crown-Tech Ltd ya Tanzania.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan leo August 04,2024 akizindua Daraja la Mto Ruaha Mkuu lenye urefu wa mita 133 na Barabara ya kiwango Cha lami kutoka Kidatu Kuelekea Ifakara yenye urefu wa Km66.9 ambayo ujenzi wake umegharimu Shilingi Bilioni 157.