September 21, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia azidi kuweka historia Mkoani Morogoro

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro ambayo alianza Agosti 2, 2024.

Ziara hiyo ni muendelezo wa ziara zake za kutembelea mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya kuzindua miradi ya kimkakati, kuhamasisha maendeleo na kitatua kero za wananchi.

Tarehe 02 Agosti 2024, Dkt. Samia
alifanya uzinduzi wa Hospitali ya Wilaya ya Gairo mradi uliogharimu Shilingi bilioni 4.8 ambapo uzinduzi huo unaashiria dhamira ya serikali kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Hospitali hiyo mpya ina lengo la kutoa huduma bora za afya na kupunguza mzigo wa kusafiri umbali mrefu kwa wananchi wa Gairo na maeneo jirani ili kupata matibabu.

Tarehe hiyo hiyo, Rais Samia alifanya uzinduzi wa Daraja la Berega, Kilosa
mradi unaotarajiwa kuboresha huduma za kijamii na kurahisisha usafirishaji wa mazao.

Daraja hilo litakuwa kiungo muhimu kwa wakulima wa Kilosa, kuwasaidia kusafirisha mazao yao kwa urahisi na kuongeza ufanisi katika masoko.

Kuhusu Umeme, Rais samia katika ziara yake aliwahakikishia wakazi wa Gairo kwamba umeme hautakatika katika tena kwani serikali imejenga ‘Substation’ wilayani kongwa ambayo itatumika mpaka Gairo

Kwa upande wa maji, Rais samia anaendelea na jukumu lake la kumtua mama ndoo kichwani kwani katika ziara hiyo amesema ndani ya jimbo hilo serikali imepeleka shilingi Bilioni 34 na mikataba mbalimbali imesainiwa ambapo tayari kazi imeanza kuhakikisha Gairo inapata maji ya kutosha.

Ndiyo maana hadi leo Rais samia anasisitiza wananchi wake waendelee kudumisha amani na utulivu ili serikali ie delee kufikiria maendeleo zaidi

Kazi anayoifanya Rais samia mkoani Morogoro inawazidi mbali wakosiaji wanaoshindwa kutambua maendeleo

Kama Agosti 3 2024, Rais Samia alizindua kampeni ya Tutunzane Mvumero hii ni katika kujali ustawi wa wananchi ambapo lengo lake ni kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji hatua inayolenga kuhakikisha amani inatawala kati ya pande hizo mbili.

Pia Rais Samia alizindua Bwawa la Umwagiliaji la kiwansa cha sukari Mtibwa, lenye mita za ujazo milioni 25 k katika kiwansa cha sukari mtibwa, wenye lengo la kuongeza uzalishaji wa sukari nchini

Mbali na hayo, Rais Samia alizindua kiwansa cha Mbegu cha Wakala wa Mbegu (ASA) na kusisitiza umuhimu wa mbegu bora katika kuongeza uzalishaji wa mazao.

Hakika Rais samia anatekeleza kwa vitendo zile ahadi alizozitoa kwa wananchi wake, na sasa wapinzani wanaendelea kukosoa bila kutoa suluhu ya matatizo ya wananchi.

Kuhusu Barabara ya Rudewa, Rais Samia amefungua barabara ya Rudewa-Kilosa yenye uredu wa Kilomita 25 itakayoongeza urahisi wa usafiri na usafirishaji wa bidhaa.

Wapinzani wako hoi hawajui nini wafanye huku Rais samia akiendelea kukatiza kila kona kulijenga Taifa kwa kutatua kero za wananchi na kuzindua miradi. Wapinzani wamebaki kubez maendeleo wakijumuisha miradi mikubwa kama SGR ambayo imeleta faida kubwa nchini

Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Morogoro imeleta matumaini mapya kwa wananchi, ikiashiria juhudi zake katika kuboresha maisha na kuleta maendeleo endelevu.

Miradi aliyoizindua ni ushahidi wa dhamira yake thabiti ya kuimarisha sekta ya afya na miundombinu, kwa manufaa ya Watanzania wote.

Na hadi sasa wakazi wa morogoro wanaendelea kumpongeza Rais samia kwa mema anayoyafanya mkoani humo.