Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya
RAIS Samia Suluhu Hassan amewaonya watendaji wa Mamlaka za maji nchini kutowakatia wananchi maji baada ya miradi inayojengwa na Serikali kwa gharama kubwa kukamilika na kuzinduliwa.
Rais Samia amesema hayo leo wakati akizindua mradi wa maji Shongo Mbalizi katika kata ya Igale wilaya ya Mbeya amesema kuwa mara nyingi maji yanaonekana siku Rais akiwepo lakini baada ya siku chache maji huwa hayatoki kabisa.
“Ndugu zangu watendaji wa Mamlaka za maji maeneo mengi tunakopita maji huwa yanatoka siku Rais anazindua mradi lakini baada ya siku tatu Rais akiondoka hayaonekani niwaombe sana watendaji serikali inatumia fedha nyingi kuleta huduma kwa wananchi na isitokee maji yakakosekana kwa wananchi na inapotokea kumetokea ukosefu wa maji toeni matangazo kwa wananchi “Amesema Rais Samia.
Hata hivyo Rais Samia amewaonya wananchi wa mji wa Mbalizi kuendelea na uzalishaji katika shughuli zote wanazofanya na kuwa mapato ya Serikali yanategemea uzalishaji wa wananchi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wizara ya Maji, Mhandisi Antony Sanga amesema kuwa mradi huo wa maji Shongo Mbalizi umeanzia chanzo cha maji Mto Shongo na mradi huo unatekelezwa una mtandao wa maji kilometa 49 na mradi umejengwa kwa thamani ya Bilioni .3.3.
Mhandisi Sanga amesema kuwa mradi huo una uwezo wa kuzalisha maji lita Mil. 8 ambao una uwezo kufika lita Mil. 12 na kuwa kwasasa wanatoa lita Mil. 8 na unahudumia wakazi wa Mbalizi 80,000.
Amesema kuwa mradi huo una uwezo wa upatikaji wa maji kwa asilimia 47 na mpaka Sasa mradi umefika asilimia 95.
Mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njenza amesema kuwa kwa muda mrefu Mji wa Mbalizi ulikuwa na changamoto ya Maji hivyo wakazi wa mji huo kunywa maji machafu hivyo uwepo wa mradi huo utakuwa msaada mkubwa Kwa wananchi.
More Stories
Serikali yaja na mwarobaini wa changamoto ya Kivuko Magogoni – Kigamboni
Kisarawe kukata keki ya Birthday ya Rais Samia
Wataalam wa afya wakutana kujadili ugonjwa wa Marburg