December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia awakonga Wafanyabishara na Sekta Binafsi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Katika mkutano wake na Baraza la Taifa la Wafanyabiashara, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa hotuba yenye matumaini makubwa kwa wafanyabiashara na wawekezaji nchini Tanzania.

Rais Samia ameeleza kwa kina hatua mbalimbali ambazo serikali yake inachukua ili kuboresha mazingira ya biashara nchini, hatua zinazolenga kuifanya Tanzania kuwa mahali pazuri zaidi kwa uwekezaji na biashara.

Rais Samia ameeleza kuhusu juhudi za serikali kuondoa vikwazo vya uwekezaji. Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kwamba taratibu zote za uwekezaji zinakuwa rahisi na zenye uwazi zaidi.

Hii itasaidia kuwavutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi, na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa letu pamoja na kuzitaka sekta mbalimbali za Kiserikali kuwa na mtazamo wa kuruhusu sera zifanye kazi na kutoa mwanya kwa sekta binafsi zijitanue katika wigo mpana kukuza ajira na kuzalisha mapato ya Serikali.