January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia awafunda Wakristo Kanisa WRM

Na Mwandishi wetu,TimesmajiraOnline, Dar

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema katika kusherekekea sikukuu ya Pasaka ni muhimu Watanzania kuyatafakari vyema mafundisho ya dini kwa kuungana na kukaa kwa wema.

Pia Rais Dkt Samia ameto pesa taslimu kwa Kanisa la WRM kama zawadi ya Pasaka kwa Kanisa hilo. Rais Samia alitoa salamu hizo alipopiga simu na kuzungumza na waumini wa kanisa hilo, jijini Dar es Salaam jana.

Dkt Samia ametoa salamu hizo Jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza kwa njia ya simu katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 17 ya Huduma za Kiroho Katika Kanisa la The Word of Recommendation Ministries (WRM) la Kivule Matembele ya pili Jijini Dar es Salaam.

Amesema Sikukuu ya Pasaka inaleta udugu wa pamoja kupitia makanisa na kukumbuka matendo ya manabii na mitume kwa kutafakari maana ya Pasaka.

“Ndugu zangu Pasaka tunayoisherekea ,wanadamu tukae kwa wema tufuate maandiko ya dini zetu na tutunze usalama wetu,”alisema Dkt Samia.

Aidha, Dkt Samia aliwatakia Pasaka njema waumuni wa Kanisa hilo na kueleza kuwa alialikwa kwenye sherehe hizo ila kutokana na majukumu ya kikazi amemtuma Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Jerry Slaa.

Kwa upande wake Waziri Slaa, aliwataka watanzania kuendelea kuwalea watoto katika malezi mema na kuacha kuchanganya mafanikio ya kiuchumi na malezi ya watoto na badala yake walehe watoto kwa kumcha Mungu.

Alisema kwa sasa jamii katika kizazi ambacho pamoja mengi ya utandawazi na mitandao huku jamii ikishindwa kutofautisha malezi na uchumi.

“Katika kitabu cha methari 22:6 neno la Mungu linatuelekeza mlee Mtoto katika njia ipasavyo naye hata iacha hata atakapokuwa Mzee.”alisema

Alisisitiza kuwa kwa sasa jamii imekuwa nyuma kuwapeleka watoto makanisani ambapo katika maeneo mengi hasa ya mjini kwenye nyumba za ibada wengi wao wamekuwa wazee na watu wazima.

Naye Nabii wa Kanisa WRM , Nicolous Suguye alimshukuru Rais Dkt Samia kwa kumpatia usajili rasmi wa Kanisa hilo .

“Tunamuombea Rais wetu azidi kuwa lulu katika ulimwenguni mzima na siasa kwa ujuml…sisi WRM tupo pamoja na nyuma yako tunakuahidi na tunafanya huduma kwa kufuata Sheria na misingi ya utulivu na kwa Tanzania nzima,”alisema Nabii Suguye