Na Mwandishi Wetu, TimesmajiraOnline, Rukwa
MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere amewataka Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha na kuchochea ajenda ya nishati safi ya kupikia nchini.
Hayo yalibainishwa na Nyerere mara baada ya uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya REA iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala, Advera Mwijage.
Amesema, Rais Samia anaendelea kuipeleka ajenda ya nishati safi kimataifa ili kuhakikisha watu wanapika katika mazingira salama kiafya na kimazingira.
Nyerere ameongeza kuwa, suala la Nishati Safi ya Kupikia sasa ni ajenda ya kimataifa na wataibeba katika kuelimisha umma kuhusu matumizi salama ya nishati hiyo kwa upana.
Kwa upande wake, Mwijage alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapika katika mazingira salama na kwamba hatua hiyo itawezekana kwa kupatikana kwa nishati safi ya kupikia iliyo nafuu inayopatikana na kutumika kwa urahisi.
Aliongeza kuwa, mtoa huduma kampuni ya Taifa Gas Limited atahudumia wilaya zilizopo ndani ya Mkoa wa Rukwa kwa kusambaza mitungi 9,765 kwa bei ya ruzuku mitungi ya gesi ya kilo sita pamoja na vifaa vyake katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji.
Alizitaja wilaya zitakazonufaika kuwa ni pamoja na Wilaya ya Kalambo, Sumbawanga na Nkasi.
More Stories
Wenje:Tuwanadi wagombea bila kuchafuana
Mtoto darasa la tatu adaiwa kujinyonga kwa kukosa nguo ya sikukuu
Jeshi la Polisi Katavi laanika mafanikio 2024