December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia atoa sadaka kwa watoto yatima

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

KATIKA kusheherekea siku yake ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Leo Ijumaa Januari 27, 2023 ametoa sadaka katika vituo vya kulelea watoto yatima vya Msimbazi na Mburahati Jijini Dar es Salaam

Akizungumza kwa niaba ya Rais Samia Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema kuwa Rais Samia ameamua kusheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kumtukuza Mwenyezi Mungu ambapo ametoa sadaka katika vituo vya kulea watoto yatima.

Aidha Ulega ametoa wito kwa viongozi wa dini kumuombea Rais Samia ili aendelee kuliongoza Taifa kwa mafanikio ambayo yameonekana kipindi hiki cha uongozi wake ikiwemo uboreshwaji wa huduma za Kijamii

Kwa upande wake Msimamizi wa kituo cha Msimbazi ‘Sister’ Stella Exavel amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa sadaka hiyo huku akibainisha kuwa wataendelea kumuombea mema na aendelee kuliongoza Taifa kwa mafanikio makubwa.