Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama kilichotokea jana mkoani Dodoma.
Katika salamu zake, amezitoa jana Rais Dkt. Samia amemuelezea marehemu Jenista Mhagama kuwa kiongozi makini, mnyenyekevu, mchapakazi na mwenye historia ndefu ya kulitumiki Taifa katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Serikali na Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Aidha, Rais Dkt. Samia ametoa pole kwa Wabunge, familia ya marehemu, ndugu na jamaa, na wananchi wa Jimbo la Peramiho, na kuwaombea moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.
“Ninatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu, wananchi wa Jimbo la Peramiho, familia, ndugu, jamaa na marafiki,”amesema Rais Dkt. Samia.

More Stories
Briquettes yaibua fursa kupunguza gharama nishati kupikia
Wananchi Arusha wapokea kwa hamasa Mkutano wa IPU
Diamond Platnumz asifu miaka 10 ya Tulia Trust