Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wapya kuongoza bodi za taasisi mbalimbali za kitaifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo unahusisha viongozi wanne walioteuliwa kushika nafasi muhimu katika bodi za mashirika ya umma.
Walioteuliwa ni pamoja na:
- Arch Dkt. Fatma Kassim Mohamed, ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kwa kipindi cha pili mfululizo.
- Balozi Dkt. Jilly Elibariki Maleko, ambaye sasa atahudumu kama Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Anachukua nafasi ya Balozi Begum Karim Taj ambaye amemaliza muda wake.
- Prof. Eliakimu Mnkondo Zahabu, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (National Carbon Monitoring Center – NCMC).
- Bw. Lucas Abrahamani Mwino, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), akichukua nafasi ya Dkt. John Kedi Mduma ambaye pia amemaliza muda wake.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Sharifa Nyanga, na kusambazwa muda si mrefu imebeba ujumbe wa kuendeleza utendaji wa taasisi hizo kupitia viongozi wenye uzoefu na weledi katika maeneo yao.
More Stories
Envaita yatambulisha mfumo wa kidigitali utoaji wa kadi za Mialiko
Wazabuni Nyanda za Juu Kusini wanolewa matumizi ya Moduli
Vipaumbele vitano Ofisi ya Msajili wa Hazina 2025/26