January 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia atengua uteuzi wa DC, DED

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wilaya hiyo, Sheilla Lukuba.

Hatua hiyo ameichukua leo, baada ya viongozi hao kushindwa kusimamia wafanyabishara wadogo wadogo maarufu kama Wamachinga mkoani Morogoro.

Rais Samia ametangaza hatua hiyo wakati akihutubia vijana wa Mkoa wa Mwanza na mikoa jirani  waliowawakilisha vijana wote nchini.

Amesema, amesikitishwa na kitendo cha Askari Mgambo katika eneo la Kituo cha Mabasi Morogoro kuwanyanyasa wafanyabishara wadogo maarufu kama Wamachinga wanaofanya biashara nje ya kituo hicho. 

Rais amesema, kitendo cha kunyanyaswa wafanyabishara hao si cha kiungwana na hakikubali kamwe.