Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan December 07,2023 ametembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko katika Mji wa Katesh Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na kuongea na Wananchi wa Katesh ambapo amewapa pole na kuwatia moyo kuwa msiba uliotokea ni wa Taifa na sio wa Manyara pekee yao huku akiwahakikishia kuwa Serikali ipo pamoja nao.
Rais Samia amesema “Ni kazi ya Mungu na hatujui Mungu katuletea hili kwa makusudi gani, kwetu sisi ni kupokea na kumshukuru hatuwezi kumlaumu na hili sio letu pekee yetu mwaka jana au mwaka juzi lilitokea Malawi tukaenda kuwasaidia nimekwenda hali ni kama hii utafikiri hakukuwa na nyumba kabisa na ni eneo kubwa, ni kushukuru na kuchukua tahadhari, sasa maeneo ya maji tuyapishe maji yachukue nafasi yake sisi tukae pembeni”
“Poleni sana kwa tukio, nimeona nije nione mwenyewe toka juzi mambo yametokea nilikuwa safari mlisikia lakini Waziri Mkuu mara moja na Serikali yote ilikuwa hapa nikawapa maelekezo nini cha kufanya wamejitahidi sana kwahiyo leo nimerudi nikaona nije mwenyewe”
“Haya ni matendo ya Mungu kwetu sisi ni kupokea na kushukuru, ingekuwa kuna Mtu kule kafungulia maji tungesema huyu Mtu huyu lakini ni Mungu mamvua yamenyesha huko yameporomosha yametokea yaliyotokea, poleni sana tupokee ni msiba wa Taifa wala sio wenu pekee yenu ni wetu sote Taifa”
“Nchi nyingine Marafiki zetu wanatoa pole sana kwa hili lililotupata, nataka niwaambie, Serikali tupo pamoja nanyi bado Mawaziri vyombo vya ulinzi na wengine wote wako hapa, tunaangalia hali halisi jinsi ya kusaidia, tunaangalia jinsi ya kuepusha Wananchi kuingie tena kwenye balaa kama hili, poleni sana Serikali tupo nanyi”
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa