Na Penina Malundo, Timesmajira Online
RAIS Samia Suluhu Hassan ameshinda nafasi ya Uwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa kura 1862 sawa na asilimia 100.
Akitangaza Matokeo hayo leo mkoani Dodoma katika Mkutano Maalum wa CCM,Spika wa Bunge ambaye Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama hicho,Job Ndugai alisema matokeo ya kura nafasi ya Uwenyekiti wa CCM Taifa amepata kura 1862 na hakuna kura iliyoharibika.
“Wajumbe wote ni 1862,waliopiga kura ni 1862 hakuna kura iliyoharibika na Mama Samia kashinda kwa kura 1862 za ndio 1862 sawa na Asilimia 100,”amesema
Wakati huo huo alisema walioshinda nafasi ya NEC ni Happiness Mgongo kwa kura 839 na Rehema Simba 867
“Katika mchakato huu wajumbe waliogombea nafasi ya Nec ni sita, wanne wakiwa wanaume na wawili wakiwa wanawake …hawa wanawake ndio wameshinda tulikubaliana 50 kwa 50 ila wanawake wamechukua 100,”Spika Ndugai
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais