Na Mwandishi Wetu, TimesmajiraOnline,Dar
RAIS Samia Suluhu Hassan, amepongezwa kwa uamuzi wake wa kutengua uteuzi wa aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Pauline Gekul.
Japo taarifa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyotolewa mwishoni juzi haikueleza sababu ya kutenguliwa kwa naibu waziri huyo, lakini Rais Samia ameungwa mkono kwa uamuzi huo, kutokana na kile kilichoelezwa kwamba kwa tuhuma zinazomkabili Gekul, hakustahili kuendelea kubaki ofisini.
Aidha, kabla ya Rais Samia kufikia uamuzi huo, baada ya kusambaa kwa video hiyo kwenye mitandao ya kijamii, wanasheria, watetezi wa haki za binadamu na wadau mbalimbali, wametaka kiongozi huyo wa umma kuwajibika mara moja au mamlaka za juu kumchukulia hatua za kinidhamu ikiwamo kutengua uteuzi wake.
“Ninampongeza Rais Samia kwa uamuzi huo, ameonesha wazi kuwa ni kiongozi anayeheshimu misingi ya utawala bora, ameamua kumuweka pembeni ili apambane na tuhuma zinazotajwa dhidi yake akiwa nje ya wadhifa wake,” amesema mmoja wa wanaharakati aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la jina lake kutochapishwa gazetii.
Amesema wakati wa Serikali ya Awamu ya Tano viongozi wengi wa Serikali walikuwa wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali, lakini waliachwa, kitu ambacho Rais Samia anaoneana kukinzana nacho, jambo ambalo limeelezwa ni zuri kwa kiongozi.
“Nimemuona kijana mmoja kwenye video akiomba msaada wa kisheria ili aweze kupeleka suala lake kwenye vyombo vya haki na kwa sababu anayemlalamikia alikuwa naibu waziri tena mwenye dhamana Wizara ya Katiba na Sheria, ili haki itendeke ni vema awe nje ya wadhifa aliokuwa nao,” amesema na kuongeza;
“Nampongeza Rais Samia ameonesha kutoka moyoni kwamba anapenda Watanzania wapate haki.”
Mwanaharakati huyo ambaye kitaaluma ni mwanasheria, anasema uamuzi huo wa Rais Samia utakuwa fundisho kwa watendaji wengine wa Serikali.
“Mtu anapokuwa kiongozi, aelewe kwamba ana dhamana nzito bila kujali ana wadhifa gani. Akituhumiwa akae pembeni ili apambane na tuhuma zake,” amesema.
Ndani ya mitandano ya kijamii kumekuwa na video inayomuonesha kijana aliyetajwa kwa jina la Hashimu Ally, akidai kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kundi la vijana kwa maelekezo ya Gekul.
Ally anadai Gekul aliamuru aingiziwe chupa sehemu ya haja kubwa au kwa madai alitumwa kimkakati kwenda Hoteli ya Paleii Lake View Garden inayodaiwa kumilikiwa na Gekul.
Kupitia mtandao mmoja wa kijamii, wakili wa kujitegemea Peter Madeleka aliandika;
“Kitendo cha kishetani alichofanyiwa Hashimu Ally, kuingiziwa chupa sehemu ya haja kubwa, siyo siasa. Tunataka wote wanaotajwa kuhusika na ushetani huu, wawajibishwe bila kujali vyeo vyao.
Aliyewahi kuwa Meya wa Ubungo, Boniface Jacob kupitia ukurasa wake wa kijamii alishauri haki itendeke.
Kwa upande wake mwanaharakati Maria Sarungi, alitaka kufanyike uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.
Katibu wa mbunge huyo inaeleza kuwa yaliyomo ndani ya videoi hiyo hayana ukweli wowote, bali kinatoendelea ni mbinu za wahutumiwa kutaka kuwatoa watu kwenye ajenda ya msingi ya tuhuma zao zinazowakabili.
Habari ambazo zimepatikana kutoka kwenye Jimbo la Babati Mjini, zinaeleza kwamba watu wengi wameunga uamuzi huo wa Rais Samia, wakisema una nia nzuri bila kujali wadhifa wa mtu.
Edward Nko, amesema kwa uamuzi huo, Rais Samia ameonesha usikivu wa kuwa kiongozi makini. Alisema viongozi waliopewa dhamana wanapokabiliwa na tuhuma mbalimbali wawajibike wenyewe, pasipo kusubiri kuwajibishwa.
Wakati wa awamu ya tano tulisikia tuhuma zilizokuwa zikiwakabili viongozi mbambali, akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ole Sabaya, lakini aliachwa ofisini, hakuguswa.
Alipokuingia madarakani aliburutwa mahakamani na ukweli ulijulikana huko huko, hivyo ndivyo inavyotakiwa, ofisi za umma hazikiwe kuwa kama kichaka,” amesema.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua