January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia apongeza ushindi wa Yanga

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

RAIS Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Yanga kwa ushindi wa
magoli manne dhidi ya CR Belouzdad ya Algeria na kutinga robo fainali
ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Rais Samia ametoa pongezi hizo jana kupitia kupitia mtandao wake wa Instagram.

“Naipongeza Klabu ya Yanga kwa kufanya vyema katika hatua ya makundi
ya Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na kufanikiwa
kufuzu hatua ya Robo Fainali.

Mafanikio haya yameandika historia kubwa kwa klabu na sekta ya michezo
nchini. Mmeleta furaha kwa mamilioni ya mashabiki wenu na Watanzania
kwa ujumla,” ameandika Rais kupitia Instagram.

Mechi ya juzikwenye Uwanja wa Mkapa, ambayo ilipewa jina la ‘Pacome
Day’ jina la mchezaji,Pacome Zouzoua ilinogeshwa na mtindo wa rangi
kwenye nywele kuanzia mashabiki, wachezaji hadi viongozi wa timu hiyo.

Baada ya mechi hiyo kumalizika Yanga ilipokea sh. milioni 20 kutoka
kwa Rais Samia kupitia kampeni ya Goli la Mama yenye lengo ya
kuhamasisha timu kufanya vizuri katika michezo ya kimataifa.