November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia anavyorudisha zama za Tanzania kusikilizwa na kuheshimika Kimataifa

*Tuna Rais wa Mabunge Duniani, Mkurugenzi wa WHO Afrika

Na Bwanku M Bwanku, Timesonline,Dar

KIHISTORIA na tangu zamani, Tanzania ni moja ya mataifa machache duniani
yaliyokuwa yanasikilizwa na kuheshimika kwa mambo mengi sana K imataifa
hasa kwa mchango wake mkubwa kwenye ukombozi wa Bara la Afrika zaidi Kusini
mwa Afrika.

Mwanamama Shupavu anayeheshimika duniani kote kama mpigania haki za wanawake duniani Gertrude Mongela aliwahi kunukuliwa akisema Tanzania ilikua ikisikilizwa na
kuheshimika sana kwenye Jumuiya za Kimataifa kiasi cha kufikia hatua kwenye mikutano ya Kimataifa watu wakisikia Mtanzania au Mjumbe kutoka Tanzania anazungumza watu wote walikua wanatega sikio kusikiliza k wa umakini Tanzania inasema nini na hata kama watu walikua wametawanyika ukumbini, wakisikia Mtanzania anataka kuongea wote wanarudi ukumbini kumsikiliza Mtanzania.

Hapo hujataja kizazi cha akina Dkt. Salim Ahmed Salim, nguli wa Diplomasia aliyetikisa na
kuheshimika duniani kote hadi kufikia nafasi ya kuwa Katibu Mkuu Umoja wa Afrika (OAU), kizazi cha Mwanamajumui Benjamin Mkapa aliyeheshimika kote
Kimataifa Kimataifa kama Mpatanishi madhubuti, akina Dkt. Anna Tibaijuka
aliyeshika hadi nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mataifa kwenye
Shirika la Makazi (UN- HABITAT) na Watanzania wengine wengi.

Hiyo ndiyo ilikua Tanzania kwenye Jumuiya za Kimataifa kwa jinsi ilivyokua
ikisikilizwa na kuheshimika japo ni ukweli usiopingika, hapa katikati ni kama
ushawishi wetu, diplomasia yetu na heshima Kimataifa
ilipungua kasi.

Sasa ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan umerudisha zama za Tanzania kusikilizwa na kuheshimika kwenye unga za Kimataifa hasa ikiwa na jambo lake.

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) , Dkt. Tulia Ackson

Baada ya Diplomasia yetu kulegalega kidogo, sasa Rais Samia amerudisha hadhi
ya Tanzania Kimataifa. Hii imethibitika kwa siku za hivi karibuni ambapo kila Tanzania ikiwa na jambo lake kwenye unga za Kimataifa imekua ikishinda kwa kishindo na kurudisha kwa kishindo zama zake za kusikilizwa na kuheshimika sana kwenye anga anga la diplomasia na Kimataifa.

Moja ya maeneo ambayo Serikali ya Rais Samia kwa miaka yake hii mitatu imeweka nguvu basi ni uhuishaji na uboreshaji mkubwa wa Diplomasia na mahusiano ya Kimataifa iliyorejesha zaidi heshima ya Tanzania iliyokua nayo toka zamani kihistoria na
kuongeza ushawishi wake mkubwa iliokuwa nao nao kwenye siasa za Kimataifa.

Kwa sasa kuongeza kusikilizwa kwake pindi inapokua na jambo lake kwenye uga wa
Kimataifa.

Nguvu kubwa ambayo Serikali ya Rais Samia imeweka kwenye diplomasia na
Mahusiano ya Kimataifa sio tu imeshusha uwekezaji mkubwa unaoshusha ajira na mapato kwa Taifa, lakini zaidi imeanza kutulipa kwa kasi kubwa sana ambapo sasa Tanzania tukiwa na jambo letu kwenye uga wa Kimataifa ni rahisi kusikilizwa
na kushinda.

Kama matokeo ya Diplomasia na mahusiano yetu kimataifa kuimarika sasa Tanzania chini ya Serikali ya Rais Samia kila tunalolitaka Kimataifa linakua
na tunashinda.

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) (WHO) Ukanda wa Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile

Ndani ya muda mfupi wa Uongozi wa Rais Samia nchi yetu imepata bahati ya kupata
nafasi mbili kubwa sana za maamuzi kwenye uwanja wa Kimataifa, nafasi zinazoongeza
fursa za maendeleo kwa Taifa letu, kusikilizwa kwetu Kimataifa na kuheshimika
maradufu.

Tanzania kwa sasa inatoa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye ni
Mtanzania Dkt. Tulia Ackson na sasa nafasi ya Dkt. Faustine Ndugulile, aliyeshinda kwenye nafasi kubwa ya maamuzi kwenye sekta ya Afya Kimataifa ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) (WHO) Ukanda wa Afrika.

Mwishoni mwa mwaka jana Oktoba 27, 2023, Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ack son alishinda na kuchaguliwa kuwa Rais wa 31 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika Kikao cha Baraza la Uongozi la Muungano huo, kilichokutana Luanda, Angola kwa kuwashinda wagombea wengine watatu na kuandika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kushika wadhifa huo mkubwa sana wenye maslahi kwa
Taifa na kuongeza nguvu ya ushawishi ya Tanzania kwenye vyombo vikubwa
vya maamuzi vya Kimataifa.

Hiyo imeongeza nguvu yetu ya ushawishi na jinsi sasa tunavyoaminiwa na kusikilizwa kwenye majambo yetu baada ya Mtanzania, Mbunge wa Kigamboni Dar es Salaam Dkt. Faustine Ndugulile kuchaguliwa pia kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
Kanda ya Afrika, nafasi inayoongeza nafasi ya Tanzania kiushawishi
kwenye sekta ya af ya duniani na kuongeza kasi yake ya kuboresha huduma
za afya k wa kutumia karata hiyo ya Mtanzania Ndugulile.

Mambo haya hayaji kwa bahati mbaya bali ni karata muhimu aliyoichanga Rais Samia kuimarisha mahusiano yetu na Mataifa ya nje kupitia safari zake za nje ya nchi na hatua zingine, ndiyo leo yanafanya Taifa letu kupata nafasi hizi kubwa zenye maamuzi
makubwa Kimataifa na zenye maslahi ya moja kwa moja kimaendeleo na kiheshima kwa Taifa