Na Agnes Alcardo,Timesmajira Online, Dar es Salaam.
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na kuongoza harambee ya kuchangia watoto wenye ulemavu wa viungo mbalimbali nchini, Agosti 18 mwaka huu.
Harambee hiyo inatarajiwa kuanza majira ya saa 12:00 jioni na inatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, itahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa dini, Wanasiasa, mashirika, taasisi na makampuni mbalimbali nchini.
Akizungumza na waandishi Dar es Salaam,leo Agosti 4,2023,Mratibu wa harambee hiyo Steve Mengele maarufu Steve Nyerere amesema kuwa Rais Samia atakuwa anafanya harambee hiyo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kuwa Rais ya nchi ya Tanzania.
Aidha Mratibu Steven amesema fedha zitakazopatikana katika harambee hiyo itakwenda kuwasaidia watoto wenye uhitaji maalum (walemavu) kununuliwa vifaa vya kusomewa na kuendelezwa kielimu, kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari na vyuo.
Naye Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki mkoa wa Tanga Dkt.Msafiri Mbilu amesema harambee hiyo itahusika kuchangia vituo hivyo vinavyosimamiwa na Dayosisi hasa katika kuwasaidia watoto hao walemavu.
Amesema vituo hivyo vinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa miundombinu ya majengo,vifaa vya kufundishia na mashine ya kusomea kwa watoto hao.
“Harambee hiyo ikifanikiwa itakuwa mkombozi wa watoto hao katika kuimarika kiafya, kielimu na kisaikolijia”amesema Askofu Mbilu.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa