December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia amteua Haniu kumrithi Msigwa

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amemteua, Jaffar Mohamed Haniu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu).

Kabla ya uteuzi huo,Haniu alikuwa Mtendaji Mkuu wa vyombo vya habari vya Africa Media Group Limited.Haniu anachukua nafasi ya Bw. Gerson Partinus Msigwa ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali. Uteuzi wa Bw. Haniu umeanza leo Juni 9, 2021.