February 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia amlilia Dkt. Sam Nujoma

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dar

RAIS Samia Suluhu Hassan, ameelezea kusikitishwa na kifo cha Rais na Muasisi wa Taifa la Namibia, Dkt. Sam Nujoma, aliyefariki, Jumamosi.

Kufuatia kifo hicho Rais Samia ametuma salamu za rambimbi akisema;

” Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda kuwasilisha salamu zetu za rambirambi kwa Rais wa Nambia, Dkt. Nangolo Mbumba, Mke wa Rais Mwanzilishi wa Jamhuri ya Namibia, Kovambo Nujoma, watoto wa Dk. Nujoma, familia yake yote, marafiki na wandugu”

Kupitia mtandao wake wa kijamii Rais Samia alisema, Dkt. Nujoma aliishi maisha ya utumishi ambayo yalitengeneza sio tu hatima ya nchi yake, bali pia kuhamasisha vizazi kusimama kwa ajili ya maadili ya uhuru, usawa na haki.

Dkt. Nujoma alifariki dunia Jumamosi Februari 8, 2025 akiwa anapatiwa matibabu nchini humo.

Taarifa za kifo chake zilitangazwa Februari 9, 2025 na Rais wa wa Namibia, Nangolo Mbumba. Sam Nujoma, atakumbukwa kwa kuiongoza Namibia kupata uhuru mwaka 1990 na kuhudumu kama Rais wake wa kwanza kuanzia 1990 hadi 2005.

“Baba yetu mwanzilishi wa Taifa, aliishi maisha marefu na yenye matokeo ambayo alitumikia kwa njia ya kipekee watu wa nchi yake anayoipenda.

Baba yetu Mwanzilishi aliwapanga kishujaa watu wa Namibia wakati wa saa za giza za mapambano yetu ya ukombozi hadi kupatikana kwa uhuru na uhuru Machi 21, 1990.

“Akiwa Rais mwanzilishi, Dk Sam Nujoma alijitoa kiuongozi kwa hali ya juu kwa taifa letu na hakuacha jitihada zozote za kuhamasisha kila Mwanamibia kujenga nchi ambayo ingesimama kidete na kujivunia miongoni mwa mataifa ya dunia,”ameandika. Rais Mbumba. Nujoma amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95