Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
RAIS Samia Suluhu Hassan, ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha Mbunge wa Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Dkt. Faustine Ndungulile,ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kupitia salamu zake, Rais Samia amesema,”Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Dkt. Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, kilichotokea usiku wa kuamkia leo Novemba 27, 2024,”amesema Dkt.Samia na kuongeza:
“Ninatoa salamu za pole kwa familia, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Tulia Ackson, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wananchi wa Kigamboni, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote.Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema,”.
Mwishoooo
More Stories
Wanaoficha watoto wenye ulemavu kusakwa
Mawakili Tabora walaani kuziwa kutekeleza majukumu
RC Mrindoko:Ufyekaji wa mahindi Tanganyika si maelekezo ya serikali