Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Majaji sita wa Mahakama ya Rufani kati yao wawili ni wanawake.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus imesema uteuzi huo umeanza Aprili 28, 2023 na kwamba siku ya kuwaapisha itatangazwa.
Miongoni mwa walioteuliwa ni Jaji Zainab Muruke, kabla ya uteuzi alikuwa Jaji Mfawidhi, Kituo Jumuishi cha Mashauri ya Ndoa, Talaka na Mirathi Temeke.
Pia amemteua Jaji Benhajj Masoud kuwa Jiaji wa Mahakama ya Rufani, kabla ya uteuzi huo, Jaji Masoud alikuwa Mkuu wa Shule ya Sheria.
Wengine walioteuliwa ni Jaji Amour Khamis kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, kabla ya uteuzi huo alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, pia amemteua Jaji Leila Mgonya, kabla ya uteuzi huo Jaji Mgonya alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Masjala Kuu Dar es Salaam.
Katika uteuzi huo wa majaji wa Mahakama ya Rufani, umewagusa Jaji Gerson Mdemu aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma na Agnes Zephania Mgeyekwa aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mhakama Kuu Divishen ya Ardhi.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu