Na Joyce Kasiki, TimesmajiraOnine, Dodoma
MKURUGENZI wa Huduma za Ushauri na Kujenga Uwezo Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Amini Mcharo, ameeleza mageuzi makubwa ya ununuzi wa umma yaliyofanyika katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu hassan .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, mcharo alisema moja ya maeneo yaliyoboreshwa ni katika mifumo, ambapo ya sh. trilioni 29 imewekwa kwenye mfumo wa NeST kwa ajili ya kufanya ununuzi wa bidhaa, huduma na kazi za ujenzi.
Alisema hadi kufikia Aprili 9, mwaka huu ,mikataba ya zaidi ya sh. trilioni 5.14 imetolewa kwa wazabuni kupitia mfumo huo, ambapo wazabuni 18,101 wamejisajili.
“Kufuatia ushiriki wa makundi maalum katika ununuzi wa umma hadi kufikia Februari 2024, jumla ya tuzo za mikataba zenye thamani ya sh. bilioni 1.95 zimetolewa kwa makundi maalum kupitia zabuni za umma zilizotangazwa na taasisi nunuzi kupitia Mfumo wa Kielektroniki (NeST),”amesema Mhandisi Mcharo na kuongeza kuwa
“Ambapo kundi la vijana wamepata tuzo za mikataba zenye thamani ya sh. milioni 709 , wanawake sh. bilioni 1.2 na wazee sh. milioni 78.3,”
Aidha, amesema katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita mamlaka ilifanya uchunguzi kwa zabuni zilizotekelezwa katika mwaka wa fedha 2021/22 na 2022/23, na kufanikiwa kuokoa jumla ya fedha za umma kiasi cha Shilingi Bilioni 16.27.
“Kati ya fedha hizo, kiasi cha sh. Bilioni 13.83 ilitokana na kuingilia kati kwa Mamlaka kwenye mikataba ambayo ilitolewa kwa wazabuni wenye bei ya juu wakati wenye bei ya chini wakitolewa kwenye mchakato na kiasi cha sh. bilioni 2.44 ni kilichorudishwa na wasambazaji wa bidhaa na wakandarasi kwa malipo ya ziada yaliyofanywa na taasisi nunuzi,” alisema Mcharo.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu