December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Nyusi arejea nchini Msumbiji

Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi ameondoka nchini baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Rasilimali Watu (Africa Human Capital Heads of State Summit) uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 na 26 Julai, 2023.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam , Rais Nyusi amesindikizwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax (Mb.), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, mhe. Faustine Kasike.