Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online,London
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema ni muhimu kuzindua mpango wa ujuzi wa vijana wa Jumuiya ya Madola ambao utatoa ujuzi kwa vijana milioni 1, katika sekta ya uchumi wa bluu na kijani ifikapo 2030.
Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo Aprili 7,2025,alipozungumza katika Mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Trade & Investment Summit 2025) kwenye ukumbi wa Jiji la kihistoria Mansion House, London.

Amehimiza kuanzishwa kwa ufadhili wa kujitolea na utaalam katika sekta hiyo ili kuharakisha maendeleo endelevu ya bahari katika nchi za Jumuiya ya Madola .
Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa washiriki wa mkutano huo kuitembelea Zanzibar na kujionea fursa za uwekezaji katika sekta ya uchumi wa buluu, utalii wa mazingira , nishati mbadala ya bahari, ufugaji wa samaki endelevu na maendeleo ya bandari.
Kwa upande mwingine, Dkt.Mwinyi amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2050, Zanzibar itakuwa ya uchumi wa kati baada ya kuzinduliwa kwa Dira ya Maendeleo kupitia mkakati wa Sera ya Uchumi wa Buluu ya mwaka 2022.
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

More Stories
Diwani awapa bima za afya watoto wa mahitaji maalum
Dkt.Mpango ashiriki dua,kumbukizi miaka 53 ya Hayati Karume
Wasira:Ilala kuna watu wameanza kampeni