Na Bakari Lulela,TimesMajira Online
MKUU wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini Tanzania, Rais mtaafu wa awamu ya pili Dkt. Alhaj Ali Hassan Mwinyi, amewasihi wahitimu wa chuo hicho kuiwakilisha vizuri jumuiya ya KIUT kwa kuwa waaminifu na waadiliifu kwa kutokushiriki katika matendo ya kifisadi ili kulipatia Taifa maendeleo.
Jumla ya wahitimu 2776 ambapo kati yao wavulana 1772 na wasichana 1004 waliohitimu katika kozi mbalimbali za Shahada ya Uzamili, Shahada, na Astashahada zinazotolewa na KIUT.
Akizungumza katika mahafali ya tatu ya chuo hicho, Mkuu wa chuo amesema anawapongeza wahitimu hao kwa hatua muhimu waliyoifikia kutokana na kusoma kwao kwa bidii na kuishi hapo chuoni kwa hali ya utulivu na maelewano muda wote wa masomo yao.
“Jamii inaamini kuwa kwa sasa mna upeo wa hali ya juu katika kupambana na changamoto zinazokwamisha maendeleo ya nchi yetu, kwa kuamini tunawatunuku vyeti vya Stashahada na shahada mbalimbali lakini uthibitisho wenu ni maarifa na ujuzi utakaotokana na utendaji wenu huko muendako,” amesema mkuu huyo
Hata hivyo amesema, anawaalika wanajumuiya ya chuo hicho sambamba na watanzania kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Rais wetu kuweza kutimiza wajibu wake kwa kufanya kazi kwa bidii na kusisitiza, kuzidi kumuombea afya njema ili watanzania na vizazi vijavyo kuendelea kunufaika na matokeo mazuri ya kazi yake.
Kupitia mahafali hayo amewaomba watu wote kuipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. Magufuli kwa kulivusha Taifa la Tanzania salama katika mapambano dhidi gonjwa hatari wa Corona, pili kwa kusimamia uchaguzi mkuu na kuchaguliwa tena kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya wadhamini Alhaj Hassan Basajj Abalaba alieleza kuwa, hivi sasa KIUT imengia mwaka wa pili wa masomo baada ya kupata ruhusa kutoka Tume ya vyuo vikuu kuweza kudahili wanafunzi kutokana na kufanyika kwa maboresho katika mfumo wa utawala na uongozi wa chuo hicho.
Kwa sasa chuo hicho hakijadili tena kuhusu kudahili wanafunzi wala kujadili walimu wasiokuwa na sifa bali hujadili maendeleo ya miundo mbinu na namna kuboresha taaluma na kukifanya kuwa na sura ya kimataifa.
Nae makamu wa chuo Profesa Jimidu Katima amesema, kipindi cha mwaka 2020, Chuo kimefundisha jumla ya kozi 30 ambapo zimeruhusiwa kufundishwa na TCU, NACTE za Astashahada na Stashahada ya kwanza ambapo kwa mwaka wa masomo uliopita chuo kilifanikuwa kutayarisha kozi 3 za uzamili.
More Stories
Jela miezi sita kwa kuvaa sare za JWTZ
Watolewa hofu uvumi juu ya uwepo wa Teleza
Tanzania,Uturuki kushirikiana kuinua sekta ya utalii nchini