Na Joyce Kasiki,TimesMajira online,Dodoma
ALIYEKAKUWA Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano Kassim Majaliwa ameteuliwa tena na Rais Dkt.John Magufuli kushika wadhifa huo.
Kabla ya kutangazwa kwa jina hilo bungeni wabunge wote walikaa kimya kuashiria shauku ya kutoka kujua jina litakalotajwa ili walithibitishe.
Spika wa Binge Job Ndugai alimwita mpambe wa rais aliyetumwa kuleta jina hilo kutoka kwa Rais Magufuli.
Mpambe huyo alimkabidhi Spika bahasha ambayo ilikuwa imegongwa mihuri sita ya siri na ndani yake kulikuwa na barua mbili ambapo moja Spika Ndugai aliisaini na kumrudishia mpambe wa Rais ambaye aliiweka kwenye begi lake na kisha kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.
Baada ya kumtaja Majaliwa kuwa ndiye aliyeteuliwa,shangwe iliibuka bungeni huku wabunge wakielekea alikokuwa amekaa mteule huyo na kumsindikiza hadi kiti cha mbele ambako alielekezwa kuketi.
Baada ya tukio hilo kukamilika,Spika Ndugai amesitisha shughuli za Bunge kwa muda ili wasifu wa mteule huyo uandaliwe na Katibu wa Bunge na kisha Bunge litarejea kwa ajili ya kulithibitisha jina hilo kwa kulipigia kura.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Rais Samia afanya uteuzi