Ikulu, Chamwino
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Mei, 2020 amekagua maandalizi ya sherehe za uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma zitakazofanyika kesho tarehe 30 Mei, 2020.
Jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi hizo litawekwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Maria Nyerere (kwa niaba ya Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere), Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Dkt. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Sherehe hizo zinatarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi na zitarushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam