Na Judith Ferdinand,Timesmajira,Online Mwanza
RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku tatu mkoani Mwanza ambapo mbali na mambo mengine ataweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR-Fela) kati ya Mwanza-Isaka.
Akizungumza leo na waandishi wa habari mkoani hapa ,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Albert Chalamila,amesema Rais  Samia Suluhu Hassan atakuwa mkoani Mwanza kuanzia Juni 13 hadi 15 mwaka huu kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Chalamila amesema,pamoja na mambo mengine Rais akiwa mkoani Mwanza atafanya shughuli mbalimbali.
Ambapo Juni 13 mwaka huu atafanya ufunguzi wa mtambo wa uchenjuaji dhahabu Mwanza na ufunguzi wa jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kanda ya Mwanza .
Juni 14 mwaka huu atazinduzi wa mradi wa maji Misungwi na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa reli ya Kisaka (SGR-Fela) kati ya Mwanza-Isaka.
Huku Juni 15 mwaka huu atatembelea na kukagua ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi pamoja na kuongea na vijana jijini Mwanza.
Amesema kwa vijana yeyote anayeona ni kijana anahamasishwa kuhudhuria kwani Rais atazungumza na vijana wote wa vyama vyote,wasio na vyama,wenye dini na wasio na dini ili kuzungumzia fursa za maendeleo.
“Hii ndio ziara yake kubwa na muhimu tangu alivyoingia madarakani,hivyo nawaomba wananchi wa Mwanza mjitokeze kwa wingi wakati wa ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Chalamila.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba