January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Dkt. Samia azidua Treni ya Umeme Dar-Dodoma

Na Mwandishi Wetu, Timesmajiraonline,Dar

RAIS Samia Suluhu Hassan, leo amesafiri na Treni ya SGR kutoka jijini Dar es Salaam hadi Dodoma kupitia Morogoro mara baada kuzindua usafiri huo kuanza kutumika nchini, tangu Tanzania ipate Uhuru mwaka 1961.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkoa wa Dodoma jana Julai 31, 2024, ilieleza kwamba Rais Samia atasafiri kwa treni hiyo kwa kilometa zaidi 444 kama ishara ya uzinduzi

Kwa mujibu wa taarifa hiyo hiyo i ni fursa kubwa ya kutangaza mazao yanayopatikana Mkoa wa Dodoma. “Kuwepo kwa treni hii ambayo kwa muda mfupi itaanza kusafirisha mazao ni fursa kubwa kwetu,” ilieleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba kutakuwa na fursa ya kibiashara kutokana na mizigo mikubwa ikiwemo makontena itakayosafirishwa kwa njia ya SGR, itashushwa katika bandari kavu iliyopo Ihumwa jijini Dodoma na kisha kusafirishwa kwenda katika maeneo mengine ndani na nje ya nchi.

“Tumejipanga Agosti Mosi 2024, kesho sisi kwetu itakuwa ni siku ya pekee ambapo mheshimiwa Rais Samia anakwenda kuzindua rasmi treni hii ya mwendo kasi, pamoja na reli ya mwendo kasi, tutakuwa zaidi ya watu 30,000 hapa kumpongeza kwa ujenzi wa reli hii,” ilifafanua taarifa hiyo.