January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Dkt. Samia awasili mkoani Mbeya kwaajili ya sikukuu ya nanenane

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt, Samia Suluhu Hassan leo August 07, 2023 amewasili Uwanja wa Ndege wa Songwe kwaajili ya kushiriki maadhimisho ya Siku ya wakulima (Nanenane) yatakayofanyika Siku ya Kesho August 08 Mkoani Mbeya.

Baada ya kuwasili Samia amepokelewa na kusalimiana na Viongozi mbalimbali waliojitokeza Uwanjani hapo kwaajili ya kumpokea.

Maonyesho ya Siku ya Wakulima Nanenane kwa mwaka 2023 yameambatana na kauli mbiu isemayo “Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mfumo endelevu wa chakula”.