Na Yusuph Mussa,Timesmajiraonline
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati anahutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 22, 2021, alijipambanua kwa kuhakikisha anamtua ndoo kichwani mwanamke wa Kitanzania kwa huduma hiyo kuwa karibu na wananchi na ikipatikana mijini na vijijini.
Na katika kuweka msisitizo, katikati ya hotuba yake bungeni, alimuamsha Waziri wa Maji Jumaa Awezo kwa kumueleza amemkabidhi wizara hiyo kwa matumaini kuwa atafikia malengo na matumaini ya Rais Dkt.Samia ya kuisaidia Sekta ya Maji kuondoa kero ya muda mrefu upatikaaji wa maji mijini na vijijini.
Matamanio ya Rais Dkt.Samia yalikwenda sambamba na kutoa fedha nyingi kwenye Sekta ya Maji, ambapo kupitia Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na mamlaka za maji mijini wameonesha kufanya kazi kubwa za kujenga miundombinu ya miradi ya maji kupitia maji ya mtiririko na ya visima (kuvuta kwa pampu) kutoka kwenye vyanzo mbalimbali.
Lakini pamoja na jitihada hizo, bado ilionekana kuna maeneo mengi ambayo hayana vyanzo vya maji ya mtiririko, lakini kama maji hayo yatatafutwa chini ya ardhi bado inaweza kuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaoishi maeneo makame ambayo hayana vyanzo vya maji ya mtiririko kabisa.
Katika kutimiza azma yake, Rais Dkt. Samia alinunua magari ya kuchimba visima na kupata maji chini ya ardhi, na kila mkoa ulipata gari moja. Na ununuzi wa magari hayo ulikwenda sambamba na kutafuta maji chini ya ardhi kwa nguvu zote.
Na hiyo ni baada ya wabunge kutoa kilio kwa Serikali kuwa, pamoja na jitihada za Serikali kujenga miradi mingi nchini, lakini bado wananchi hasa wa vijijini, wanatafuta maji kwa umbali mrefu, huku, na hasa wanawake wakihatarisha maisha yao na ndoa zao kwa ajili ya kutoka usiku wa manane kutafuta maji.
Ndipo Rais Dkt. Samia alipokuja na mpango wa kuchimba visima 900 kwenye majimbo 180 nchini ili kuona wanapunguza kama sio kuondoa kabisa tatizo la maji na hasa vijijini.
Hivyo, kufanya miradi ya maji kwenda vijijini isiweze kukwama, kama eneo husika halina vyanzo vya maji vya mtiririko, maji hayo yalitafutwa chini ya ardhi.
Mwandishi wa makala haya alizungumza na Meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Dodoma Mhandisi Mbaraka Ally na kueleza miradi iliyoanza kutoa huduma na iliyokamilika katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia,Lakini pia alieleza miradi inayotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
MIRADI ILIYOKAMILIKAI NA KUANZA KUTOA HUDUMA
Katika Wilaya ya Bahi, ukiacha miradi midogo midogo ya wafadhili ikiwemo kukarabati miradi ya zamani ili wananchi wapate maji, lakini ipo miradi mikubwa nayo imekamilika. Ujenzi wa Mradi wa usambazaji maji Chikola. Mradi huo uliopo Kijiji cha Chikola unanufaisha wananchi 3,720, ukiwa umejengwa kwa gharama ya sh. milioni 342,750,000, na ukiwa na vituo vys kuchotea maji (vilula) 16, na tenki lenye ujazo wa lita 30,000.
Mradi wa Maji wa Kisima cha Ndege. Upo Kijiji cha Kisima cha Ndege, wanufaika wakiwa 5,324, ukiwa na vilula 10, tenki la ujazo wa lita 40,000, na umejengwa kwa gharama ya sh. 598,187,737.Mradi wa Maji Lamaiti, utahudumia wananchi 7,194, ukiwa na vilula 23, ujazo wa tenki lita 70,000, na umejengwa kwa gharama ya sh. 835,591,980. Uchimbaji wa kisima na ujenzi wa kituo cha kuchotea maji Kijiji cha Mnase, ambapo wananchi 4,856 wa Kijiji cha Mphangwe watanufaika na mradi huo uliogharimu sh. 477,685,800, ukiwa na vilula 13 na tenki la ujazo wa lita 40,000.
Mradi wa Maji Chifutuka, huo utahudumia wananchi 11,000 wa Kijiji cha Chifutuka, na kuwa na vilula 23, tenki la lita 80,000, ukigharimu sh. milioni 812.6. Mradi wa Maji Kijiji cha Mzogole utahudumia wananchi 6,484, ukiwa na vilula 18, na tenki la lita 40,000, ukijengwa kwa sh. milioni 632.
WILAYA YA CHAMWINO
Wilaya ya Chamwino, ujenzi na upanuzi wa Mradi wa Maji Mlowa bwawani. Mradi huo utahudumia wananchi wa Kijiji cha Mlowa Barabarani wapatao 8,358. Mradi umejengwa kwa gharama ya sh. 213,439,260, huku ukiwa na tenki la lita 90,000. Ujenzi na ukarabati wa mradi wa usambazaji maji katika Kijiji cha Iringamvumi. Mradi huo utanufaisha wananchi wa vijiji vitatu vya Iringa Mvumi Zamani, Iringa Mvumi Mpya na Chita wapatao 8,221, ukiwa na vilula 12, tenki la lita 100,000, na umegharimu sh. 432,618,934.
Ujenzi wa Mradi wa Maji Kijiji cha Dabalo.. Utahudumia wananchi 8,188, na una vilula 18, tenki la lita 150,000, ukigharimu sh. 906,792,586. Mradi wa Maji Kijiji cha Manchali utahudumia wananchi 3,260, vilula 20, tenki lita 135,000 na umegharimu sh. 542,506,260.
WILAYA YA CHEMBA
WIlaya ya Chemba, upo mradi wa uwekaji wa tenki, pampu, mfumo wa umeme wa jua, uwekaji wa mabomba katika vijiji vya Muungano, Chukuruma na Maziwa. Wananchi 8,971wa vijiji hivyo watanufaika kwa mradi huo uliowekwa vilela vitatu na tenki la lita 150,000.
Mradi wa kusambaza maji ya pampu katika Kijiji cha Hania, na ukarabati wa skimu ya usambazaji maji ya Songolo. Wananchi wa vijiji vya Hania na Songolo wapatao 8,282 watanufaika. Mradi una vilula 11, tenki la lita 125,000, na kugharimu sh. 251,950,816. Upanuzi wa ukarabati wa Mpango wa Maji wa Mji wa Chemba, ambapo wananchi 12,084 wa vijiji vya Chambalo na Chemba watanufaika, na wamewekewa vilula viwili na tenki la ujazo wa lita 150,000, na kugharimu sh. 756,701,838.
WILAYA YA KONDOA
Wilaya ya Kondoa. Mradi wa Maji Kwahengwa ambao utahudumia wananchi 3,225 wa vijiji viwili vya Kwahengwa na Sakami, umegharimu sh. milioni 272, ukiwa na vilula 18, na tenki la lita 100,000. Mradi wa Maji Bukulu. Huo unanufaisha wananchi 5,499 ukiwa umejengwa kwa gharama ya sh. 451,572,102, na una vilula saba na tenki la ujazo wa lita 140,000. Mradi Kikore- Mkurumuzi utanufaisha wananchi 5,878 wa vijiji vya Kikore na Mkurumuzi, umewekewa vilula 13 na tenki la ujazo wa lita 150,000.
Mradi wa usambazaji Kijiji cha Bicha, wananchi 2,869 watanufaika, huku kukijengwa tenki la ujazo wa lita 250,000, vilula vitatu, na kugharimu sh. 596,986,317.
WILAYA YA KONGWA
Wilaya ya Kongwa, kuna Mradi wa Maji Kijiji cha Mkoka, wananchi 13,249 watanufaika, baada ya kuwekewa vilula 16, tenki la lita 135,000. Mradi wa Maji Kijiji cha Laikala B utahudumia wananchi 3,882 waliowekewa vilula tisa na tenki la lita 100,000, huku ukigharimu sh. 780,566,436. Usambazaji wa vifaa vya ujenzi vijiji vya Sejeli, Manyata na Laikala A (PbR V), ambapo vijiji vitatu vya Sejeli, Manyata na Laikala A vyenye wakazi 11,357 vitanufaika. Kumewekwa vilula vinne (4), na ujenzi kugharimu sh. 110,020,951. Ujenzi Mradi wa Maji Kijiji cha Mgoroka umegharimu sh. 147,504,830, ukiwekewa vilula viwili na tenki la lita 50,000, na wananchi 1,718 watanufaika.
WILAYA YA MPWAPWA
Wilaya ya Mpwapwa. Ujenzi wa Mradi wa Maji Kidenge- Luhundwa na Mpwanila. Mradi huo utahudumia wananchi 8,897 wa vijiji vya Luhundwa, Kidenge na Mpwanila. Wamewekewa vilula 32, na mradi umegharimu sh. 1,070,460,730.
Ukarabati na uboreshaji wa Skimu ya usambazaji maji ya UVIKO 19 wa Kibakwe. Mradi utanufaisha wananchi 9,878 wa Kijiji cha Kibakwe. Mradi huo uliogharimu sh. milioni 500, una kituo cha kuchota maji kimoja na tenki lenye ujazo wa lita 200,000.
Ujenzi wa Skimu ya Usambazaji maji Kijiji cha Mima, ambapo wananchi 5,557 wa vijiji vya Mima na Igoji II watanufaika kwa kuwekewa vilula 11 na tenki la ujazo wa lita 100,000. Ujenzi wa pampu ya usambazaji maji katika Kijiji cha Iyoma, wananchi 5,712 watanufaika baada ya kuwekewa vilula tisa, tenki la lita 75,000, ukigharimu sh. 409,053,977. Ujenzi wa pampu ya usambazaji maji Skimu ya Kijiji cha Kibakwe, wananchi 3,092 watanufaika kwa kuwekewa vilula tisa na tenki la lita 50,000 na kugharimu sh. 478,604,719.
Ukarabati na uboreshaji wa mradi wa maji Chipogoro ambao utanufaisha wananchi 6,547 wa vijiji vya Chipogoro na Chinoje, na wamewekewa vilula 27 na tenki la lita 50,000, huku mradi huo ukigharimu sh. milioni 87. Ujenzi wa Mradi Kijiji cha Iramba, utanufaisha wananchi 1,222 baada ya kuwekewa tenki la lita 75,000 na vilula vitano. Ujenzi wa pampu ya usukumaji maji katika Kijiji cha Kibagwe iliyojengwa kwa gharama ya sh. 478,604,719, na watu 3,092 watanufaika.
MIRADI INAYOTEKELEZWA 2024/2025
Wilaya ya Bahi. Ujenzi wa Mradi wa Maji Ibihwa utanufaisha wananchi 7,443, na utagharimu sh. 709,317,420. Ujenzi wa Mradi wa Maji vijiji vya Chali Makulu, Chali Isanga na Chali Igongo utanufaisha wananchi 8,678, na unajengwa kwa gharama ya sh. 2,505,608,432. Mradi wa Maji vijiji vya Kigwe na Mapinduzi utahudumia wananchi 8,202, na utagharimu sh. milioni 300.6.
Ujenzi wa Bwawa la Chikopelo linalojengwa kwa gharama ya sh. 2,897,336,937 litanufaisha vijiji vya Chikopelo, Chipanga A, Chipanga B, Chikola, Nghulugano, Chimendeli, Bahi Makuli, Bahi Mjini.Utafiti wa maji chini ya ardhi, uchimbaji wa visima vinane (8) vya Nkhome, Bahi Makulu, Lukali, Chipanga A (Sulughai), Nondwa (Chihundiche), Tinai (Isangha), Kongogo (Mkalama), Makanda (Chidete), utanufaisha vijiji vya
Nkhome, Bahi Makulu, Lukali, Chipanga A (Sulughai), Nondwa (Chihundiche), Tinai (Isangha), Kongogo (Mkalama), Makanda (Chidete). na utagharimu sh. 261,640,000.
Ujenzi wa Mradi wa Maji Nagulo Bahi utakaohudumia vijiji vya Bankolo, Mpamantwa, Nagulo Bahi, Iwumba na Ikumbulu utahudumia vijiji sita, na idadi ya watu 29,989 watanufaika, na utagharimu sh. 368,216,000. Mradi wa Maji Asanje utahudumia wananchi 2,887, na utagharimu sh. milioni 450, Mradi wa Maji Isangha utahudumia wananchi 6,493 na utagharimu sh. milioni 539, Mradi wa Maji Nagulo Bahi utahudumia wananchi 9,437, na utagharimu sh. milioni 880, Mradi wa Maji Ilindi wananchi 7,382 watanufaika, na gharama ya mradi ni sh. milioni 770, na ujenzi wa Mradi wa Maji Msisi utahudumia wananchi 6,500 kwa gharama ya sh. milioni 200.
WILAYA YA CHAMWINO
Ujenzi wa Mradi wa Maji Kijiji cha Mheme/Chikola, utanufaisha wananchi 2,589 wa Kijiji cha Mheme, na kugharimu sh. milioni 400.5. Mradi wa Maji Kata ya Mvumi Mission utahudumia wananchi wa vijiji vya Mvumi Mission, Chihembe na Mila, vikiwa na wananchi 8,361 na utagharimu sh. 988,821,460. Mradi wa Maji vijiji vya Handali na Mjelu utahudumia wananchi 5,157, kwa gharama ya sh. 698,201,794, na Mradi wa Maji Kijiji cha Izava (Wali) utahudumia wananchi 1,212, na utagharimu sh. 398,741,316.
Ujenzi wa Mradi wa Maji Nagulo utahudumia wananchi 5,192, na kugharimu sh. 282,848,628, Mradi wa Maji Kijiji cha Haneti utagharimu sh. 920,131,756, na kuhudumia wananchi 7,920, Mradi wa Maji Kijiji cha Mgunga utanufaisha wananchi 2,881, na gharama ni sh. 276,620,980. Mradi wa Maji Kijiji cha Mlowa Barabarani utahudumia wananchi 3,296, na kugharimu sh. 329,382,083, na Mradi wa Maji Kijiji cha Magungu utahudumia wananchi 2,881, na gharama ni sh. 277,616,682.
WILAYA YA CHEMBA
Mradi wa Maji Kijiji cha Machiga- Changamka utahudumia wananchi wa vijiji viwili wapatao 15,649 kwa gharama ya sh. milioni 730. Mradi wa Maji Kijiji cha Chandama utahudumia wananchi wa vijiji viwili, Chandama na Mpendo wapatao 6,669 na utagharimu sh. 555,384,640. Mradi wa Maji Kijiji cha Khubunko utahudumia wananchi 2,786 kwa gharama ya sh. 330,617,919. Na Upanuzi na ukarabati Mradi wa Maji katika vijiji vya Huwekwa, Mlongia, Chinyika, , Kubi, Kwamtoro, Soya, Dalai, Daki, Churuku na Gumbu utahudumia vijiji tisa vyenye wakazi 43,584, na utagharimu sh. 690,342,635.
Utafiti wa maji chini ya ardhi na uchimbaji wa visima 11 katika vijiji vya Cheku A, Ombiri, Mbarada, Madaha, Majengo Mapya, Tumbakose, Sankwaleto, Ndoroboni, Manantu, Binse na Mpendo kugharimu sh. milioni 505,449,637. Mradi wa Maji Kelema- Balai utahudumia vijiji viwili vyenye wakazi 6,659 kwa gharama ya sh. 575,183,014. Usambazaji wa malighafi na bomba na viungo vya bomba katika ukarabati wa Mradi wa Maji Kelema Maziwani na Ovada, utahudumia wananchi 6,713 kwa gharama ya sh. 438,149,820. Mradi wa Maji Kijiji cha Igunga utahudumia wananchi 3,637, na kugharimu sh. milioni 360.
Mradi wa Maji Kijiji cha Kelema Huwekwa, utahudumia wananchi 1,937 kwa gharama ya sh. milioni 365. Mradi wa Maji Kijiji cha Mwailange utahudumia wananchi 7,483 kwa gharama ya sh. 616,364,504. Mradi wa Maji Kijiji cha Mrijo Juu, utahudumia vijiji vitatu vya Mrijo Juu, Olboloti na Mrijo Chini vyenye wakazi 10,725, na utagharimu sh. milioni 800.
WILAYA YA DODOMA
Mradi wa Maji Mapinduzi B utakaogharimu sh. 468,078,000, utanufaisha wananchi 9,383. Mradi wa Maji Mayeto na Hombolo Makulu utahudumia wananchi 8,283 kwa gharama ya sh. 512,230,333. Mradi wa Maji Chikowa utahudumia wananchi wa vijiji vinne vya Chikowa, Bihawana, Iwelewele, na Mapinduzi wapatao 10,693, na utagharimu sh. 568,354,994. Utafiti wa maji chini ya ardhi, na uchimbaji visima viwili Nkulabi na Mahona Makulu, kusafisha kisima na kufanya upimaji wa wingi wa maji utagharimu sh. milioni 84,246,667. Na ukarabati wa Mradi wa Maji Ipala utakaohudumia wananchi 3,516, utagharimu sh. milioni 14.4.
WILAYA YA KONDOA
Ukarabati wa Mradi wa Maji vijiji vya Sauna na Mapinduzi vyenye wakazi 2,234, utagharimu sh. 913,320,252. Ujenzi wa Mradi wa Maji Pahi, utahudumia vijiji viwili vya Pahi na Ikova vyenye wakazi 6,768, na kugharimu sh. 937,877,030. Mradi wa Maji Kijiji cha Kisaki chenye wakazi 4,452 utagharimu sh. 572,085,660. Mradi wa Maji Kijiji cha Baura chenye wakazi 2,219 mradi kugharimu sh. 700,609,870. Mradi wa Maji Kijiji cha Kikilo Kati kuhudumia wananchi 4,444 kwa gharama ya sh. 396,712,504. Mradi wa Maji Mauno kujengwa kwa gharama ya sh. 489,195,353, na kunufaisha wananchi 7,574. Mradi wa Maji Soera kujengwa kwa gharama ya sh. 278,390,110, na kuhudumia wananchi 2,713.
Ujenzi wa Mradi wa Maji Sambwa kuhudumia wananchi 29,243 wa vijiji sita vya Sambwa, Idindiri, Keikei, Ihari,Keikei Tangini na Ikengwa, na kugharimu sh. 3,155,324,424. Bwawa la Itaswi- Kisaki kugharimu sh. 5,700,884,713. Mradi wa Maji Kwamafunchi kuhudumia wananchi 2,219, na kugharimu sh. 809,537,820. Mradi wa Maji Madege kuhudumia wananchi 3,124, na kujengwa kwa gharama ya sh. 470,397,532. Mradi wa Maji Masawi kugharimu sh. 1,160,433,839. Na utaweza kuhudumia wananchi wa vijiji vinne vya Masawi, Bereko, Lembo na Alagwa wapatao 10,806.
Ujenzi wa Mradi wa Maji Kikore na Mkurunzi, utahudumia wananchi 4,413, na utagharimu sh. 889,241,348. Mradi wa Maji Bambare kuhudumia wananchi 3,692, na utagharimu sh. 1,270,494,630. Mradi wa Maji Itundwi kuhudumia wakazi 3,592, na gharama ya mradi ni sh. 784,159,091. Mradi wa Maji Hachwi, wananchi 2,470 kunufaika, na utagharimu sh. 803,911,272. Mradi wa Maji Mulua una wakazi 6,958, na utagharimu sh. 872,866,209. Mradi wa Maji Kilimani utagharimu sh. 706,556,681, na utanufaisha wananchi 4,316.
Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Mji wa Kondoa utanufaisha wananchi 24,674 kwenye vijiji saba vya Mnarani, Maji ya Shamba, Iboni, Chemchemi, Miningani, Kichangani na Ubembeni, na utagharimu sh. 4,094,604,597. Mradi wa Maji Tampori, Gubali na Choka utahudumia wananchi 5,316 na utagharimu sh. 1,025,725,050. Ujenzi wa miradi midogo (Point Source) katika vijiji vya Matangalimo, Nanakwi B, Ikengwa, Mkundulu na Hurui kuhudumia wananchi wa vijiji vitano na utagharimu sh. 222,335,159.
Ujenzi wa miradi midogo (Point Source) katika vijiji vya Masange, Ntomoko, Filimo, Changaa, Changaa Sekondari, Madege, Mitati, Salanka, Itundwi na Haubi. Wananchi wa vijiji 10 watakaonufaika, na mradi utagharimu sh. 184,234,782. Ujenzi wa vichoteo vinane katika vijiji vya Munguri, Dumi, Hurumbi, Msui na Chora, wananchi wa vijiji vitano watanufaika, na utagharimu sh. 221,299,277. Mradi wa Maji Kisesa Sauna na Kikore, wananchi wa vijiji viwili wapatao 5,878 kunufaika, na utagharimu sh. 184,234,782.
WILAYA YA KONGWA
Mradi wa Maji Masinyeti ambao utagharimu sh. 797,192,950, na kunufaisha wananchi 3,546. Utafiti na uchimbaji wa visima tisa kwenye vijiji vya Silale, Chiwe, Mahutya, Chang’ombe, Ngoma, Nyerere, Magereza (Manyata), Wenzamtima, Muungano (Songambele). Mradi utagharimu sh. 436,545,000.
Utafiti na uchimbaji wa visima 16 kwenye vijiji vya Lengali, Kinangali, , Bwawani, Njoge, Masenha, Silwa, Mbande, Idido, Mangweta, Ihanda, Lobilo, Soiti, Chitego, Wangazi, Matanga na Mgoloka. Mradi huo utagharimu sh. 735,199,472. Mradi wa Maji Chinanjilizi, utahudumia wananchi 1,502, na utagharimu sh. 490,488,617. Mradi wa Maji vijiji vya Chamkoroma na Makole utahudumia wananchi 7,235, na utagharimu sh. 542,100,904. Mradi wa Maji Ijaka kuhudumia wakazi 4,004, na utagharimu sh. 417,305,904.Mradi wa Maji Mangweta unajengwa kwa gharama ya sh. 68,333,800, na wananchi 2,143 watanufaika.
Ujenzi wa Mradi wa Maji Matanga na Ngutoto utanufaisha wananchi wa vijiji viwili wapatao 6,018, na unatekelezwa kwa gharama ya sh. 95,934,000. Mradi wa Maji Songea mbele na Masenha unaojengwa kwa gharama ya sh. milioni 556.8, utanufaisha wananchi 17,823. Na Mradi wa Maji Mtanana B, utahudumia wananchi 4,088, na unajengwa kwa sh. 103,983,378.
WILAYA YA MPWAPWA
Ujenzi wa Mradi wa Maji Chinyika- Mlunduzi. Utahudumia wananchi wa vijiji viwili wapatao 8,176, na utatekelezwa kwa gharama ya sh. 967,668,470. Mradi wa Maji Kijiji cha Igoji I. Utahudumia wananchi 6,183, na utagharimu sh. 430,553,311. Mradi wa Maji Lupata- Makutupa, utahudumia wananchi wa vijiji viwili wapatao 9,286, na utagharimu sh. 2,527,100,461. Mradi wa Maji ambao utahudumia wananchi wa vijiji vinne vya Pwaga, Munguwi, Maswala na Itende wapatao 18,599, utagharimu sh. 4,303,281,669.
Ujenzi wa miundombinu ya tenki la maji na ofisi Mradi wa Maji Mtera, kunufaisha wananchi 6,476, na utagharimu sh. 1,783,973,588. Mradi wa Kijiji cha Gulwe utanufaisha wananchi 5,832, na utagharimu sh. 628,683,958. Upanuzi wa Mradi wa Maji kutoka Pwaga kwenda Idaho. Utahudumia wananchi 1,415, na kugharimu sh. milioni 356. Upanuzi wa Mradi wa Maji Lupeta- Makutupa kwenda Kijiji cha Inzomvu, utahudumia wananchi 7,349, na unajengwa kwa sh. milioni 370. Mradi wa Maji Berege Sekondari unajengwa kwa sh. milioni 156 na utanufaisha watu 1,000.
Ujenzi wa Mradi wa Maji Kijiji cha Mwanawota, unatekelezwa kwa sh. milioni 650, na utahudumia wananchi 3,970. Mradi wa Maji Kijiji cha Chaludewa unajengwa kwa gharama ya sh. milioni 450, na utahudumia wananchi 3,472. Mradi wa Maji Kijiji cha Mzogole, wananchi 2,107 watanufaika, na unajengwa kwa gharama ya sh. milioni 180.
Ukarabati wa Mradi wa Maji Kijiji cha Chinyanhuku unaotekelezwa kwa sh. milioni 155, utahudumia wananchi 4,445. Upanuzi wa Mradi wa Maji Luhundwa Chang’ombe, unajengwa kwa sh. milioni 200, na utahudumia wananchi 1,456. Mradi wa Maji Pandambili, unatekelezwa kwa sh. milioni 210, na utanufaisha wananchi 1,212. Upanuzi wa Mradi wa Maji Kisokwe- Idilo Mazae, utahudumia vijiji vitatu vyenye wakazi 6,662, na utagharimu sh. milioni 864. Na utafiti wa maji ardhini na uchimbaji wa visima virefu vijiji vya Chimaza, Nana na Mkanana Chibwegere. Utagharimu sh. milioni 135.
More Stories
Ubunifu wa Rais Samia kupitia Royal Tour unavyozindi kunufaisha Tanzania
Rais Samia anavyojenga taasisi imara za haki jinai kukabilina na rushwa nchini
Rais Dk. Samia alivyowezesha Tanzania kuwa kinara usambazaji umeme Afrika